Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI

Putin na Biden kukutana Juni 16 Geneva

Marais wa Marekani Joe Biden na Urusi Vladimir Putin watakutana Juni 16 huko Geneva, Uswisi, White House na Kremlin wametangaza Jumanne hii, katikati mwa mvutano kati ya Washington na Moscow kuhusu maswala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuingiliwa kwa uchaguzi na uharamia wa kimtandao.

Raiswa Marekani Joe Biden (kushoto) akiwa na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin (kulia).
Raiswa Marekani Joe Biden (kushoto) akiwa na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin (kulia). AP - Alexander Zemlianichenko
Matangazo ya kibiashara

Shirika la habari la REUTERS liliripoti mapema mwezi huu kwamba Marekani na Urusi hazikuwa na matarajio maalumu kwa mkutano huo, kwa kuuona zaidi, kulingana na vyanzo kadhaa, kama fursa ya kupunguza mivutano badala ya kila upande kuonyesha msimamoa wake.

"Viongozi watajadili maswala mbalimbali muhimu, wakati tunajaribu kurejesha mazingira bora na utulivu katika uhusiano kati ya Marekani na Urusi," msemaji wa White House almesema Jumanne hii, akiongeza kwamba Ukraine na Belarus zitakuwa kwenye agenda ya mazungumzo yao.

Hakuna sharti ambalo limewekwa kwa mkutano huu, amebainiJen Psaki kwa waandishi wa habari.

Kremlin, kwa upande wake, imesema katika taarifa kwamba marais wa Urusi na Marekani watajadili uhusiano wa nchi hizo mbili, maswala yanayohusiana na utulivu wa kimkakati wa nguvu za nyuklia na maswala mengine ikiwa ni pamoja na ushirikiano katika mapambano dhidi ya janga la Corona na mizozo ya kikanda.

Katika siku za hivi karibuni, Joe Biden alisema anataka Vladimir Putin aache kujaribu kuingilia uchaguzi wa Marekani, kukomesha mashambulizi ya kimtandao kwenye mitandao ya Marekani, kutotishia uhuru wa Ukraine na kumwachilia mpinzani wa Urusi, Alexei Navalny.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.