Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI

Marekani na Urusi wajianda kwa mkutano wa Joe Biden na Vladimir Putin

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov wanatarajia kukutana Jumatano jioni kukubaliana juu ya mkutano wa marais kutoka nchi hizo mbili licha ya uhusiano mgumu kati ya nchi zao.

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari,
Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari, SAUL LOEB POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo ambayo yatafanyika kando ya mkutano wa mawaziri wanane wa mambo ya nje huko Reykjavik, utakuwa mkutano wa ngazi ya juu tangu Rais wa Marekani Joe Biden aingie madarakani mwezi Januari.

Uhusiano kati ya nchi hizi mbili umedorora tangu mwezi Machi, wakati Joe Biden, alipoulizwa na kituo cha ABC kusema ikiwa anafikiria Vladimir Putin ni muuaji, alijibu "ndio", na kuongeza kuwa kiongozi wa Urusi hana moyo wa kiutu. Kauli hii ilisababisha Moscow kumuitisha nyumbani balozi wake nchini Marekani kwa mashauriano ya haraka juu ya mustakabali wa uhusiano kati ya Washington na Moscow.

Marekani baadaye iliweka vikwazo kadhaa dhidi ya Urusi kuadhibu kile ilichokielezea kama mfululizo wa vitendo "vibaya", pamoja na madai ya kuingiliwa kwa uchaguzi wa urais wa Marekani mezi Novemba mwaka uliyopita.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Ned Price amesema Sergei Lavrov na Antony Blinken watakutana Jumatano hii jioni baada ya mkutano wa Baraza la Aktiki, kundi la mataifa manane.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.