Pata taarifa kuu
ITALIA

Coronavirus: vifo 380 na visa vipya 24,000 vyaripotiwa Italia

Italia imerekodi vifo vipya 380 leo Jumamosi kutokana na ugonjwa wa CoOVID-19 dhidi ya 457 siku iliyotangulia, Wizara ya Afya imetangaza, wakati idadi ya visa vpya vya maambukizi imepungua kidogo hadi 23,839 dhidi ya 23,987 siku iliyopita.

Kituo cha chanjo ya Covid-19, katika uwanja wa ndege huko Roma, Italia, Machi 8, 2021.
Kituo cha chanjo ya Covid-19, katika uwanja wa ndege huko Roma, Italia, Machi 8, 2021. © REUTERS - GUGLIELMO MANGIAPANE
Matangazo ya kibiashara

Italia imerekodi vifo 107,636 kutokana na COVID-19 tangu kuzuka kwa janga hilo mnamo mwezi Februari mwaka jana ikiwa ni idadi kubwa ya  vifo barani Ulaya baada ya Uingereza. Zaidi ya kesi milioni 3.5 zimerekodiwa hadi sasa.

Katika muda wa saa 24 zilizopita, watu 264 wamelazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi, ikiwa ni idadi ya chini ya ikilinganishwa na idadi ya wagonjwa 288 waliolazwa siku ya Ijumaa, na kufanya idadi ya watu waliolazwa hospitalini katika wodi ya wagonjwa mahututi kufikia 3,635 dhidi ya 3,628 siku iliyotangulia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.