Pata taarifa kuu
ITALIA-CORONA-AFYA

Coronavirus Italia: Hatua mpya za kuzuia maambukizi zaanza kutumika Jumatatu

Italia merekodi visa vipya 11,705 vya maambukizi ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Covid-19 siku ya Jumapili na vifo 69 katika muda wa saa 24 baada ya watu 10,925 kuambukizwa virusi hivyo Jumamosi na vifo 47 kuthibitishwa.

Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte (hapa alikuwa Brussels Oktoba 16, 2020) alitangaza hatua mpya za kupambana na virusi vya Corona Jumapili.
Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte (hapa alikuwa Brussels Oktoba 16, 2020) alitangaza hatua mpya za kupambana na virusi vya Corona Jumapili. REUTERS/Johanna Geron
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, takwimu hizi bado ziko chini sana kuliko ripoti za kila siku wakati wa rekodi ya janga hilo mwezi Machi na Aprili. Ili kuepeka masharti mapya ya watu kutotembea, serikali haitaki kupoteza wakati. Makata mapya yanaanza kutumika leo Jumatatu.

Mikoa ya Milan, Naples na Roma imethiriwa zaidi na ongezeko la maambukizi haya. Na viashiria vya afya vinazorota kila mahali. Kutokana na hali hiyo Waziri Mkuu Giuseppe Conte alitangaza makata mapya ya kuvaa barakoa za kitabibu: "Hatuwezi kupoteza wakati. Lazima tuchukue hatua kwa kutekeleza hatua zote muhimu za kuepuka kurudi kusalia manyumbani, hali ambayo itaathiri uchumi wote wa nchi. "

Miongoni mwa hatua kuu, agizo hilo linatoa mwanya zaidi kwa mameya wa miji yote, ambao wataweza kutangaza hatua kuhusu saa za watu kutotembea. Migahawa itafungwa usiku wa manane na kukaa watu sita tu kwa kila meza. Baa, bila huduma ya upishi, italazimika kufungwa kuanzia saa 12 jioni hadi saa 11 asubuhi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.