Pata taarifa kuu
ITALIA

Coronavirus: Uvaaji barakoa ni lazima kote Italia

Italia imechukua hatua ya kuwataka raia wake kuvaa barakoa wakiwa nje ya makwao katika lengo la kupambana na janga la COVID-19 linalosababishwa na virusi vya Corona, Wizara ya Afya imetangaza kufuatia idhni ya serikali kwa hatua hii.

Ugonjwa wa COVID-19 umesababisha vifo vya zaidi ya watu 36,000 nchini Italia, chanzo cha serikali kimebaini.
Ugonjwa wa COVID-19 umesababisha vifo vya zaidi ya watu 36,000 nchini Italia, chanzo cha serikali kimebaini. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Italia inakabiliwa na ongezeko la maambukizi ya kila siku ya virusi vya Corona, lakini kwa kiwango kidogo ikilinganishwa na nchi zingine za Ulaya kama Ufaransa, Uhispania au Uingereza.

Serikali ya Italia pia imeamua leo Jumatano kuongeza muda wa hali ya dharura iliyotangazwa dhidi ya COVID-19 hadi Januari 31.

Ugonjwa wa COVID-19 umesababisha vifo vya zaidi ya watu 36,000 nchini Italia, chanzo cha serikali kimebaini.

Wakati huo huo mamlaka nchini Ubelgiji imechukuwa hatua ya kufunga kwa kipindi cha mwezi mmoja baa na mikahawa katika mji mkuu wa nchi hiyo. Hatua hiyo itaanza kutumika Alhamisi wiki hii kwa sababu ya kuzuka kwa visa vipya vya maambukizi ya visa vya Corona.

Pamoja na  kiwango cha maambukizi ya visa vipya 502 kwa wakaazi 100,000 katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, mji mkuu wa Ubelgiji unaongoza dhidi ya mji mkuu wa Ufaransa, Paris, na sasa unashika nafasi ya pili kati ya miji mikuu ya wanachama 27 wa Umoja aw Ulaya kwa kigezo hiki, nbaada ya Madrid.

Rudi Vervoort, Waziri na rais wa mkoa wa Brussels, amesema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba baa na mikahawa yote, ikiwa pamoja na vituo vinavyotoa huduma ya kahawa au chai, vitafungwa kuanzia Alhamisi wiki hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.