Pata taarifa kuu
ITALIA-CORONA-AFYA

Idadi ya visa vipya 1,733 vyathibitishwa Italia

Italia imerekodi visa vipya 1,733 vya virusi vya maambukizi ya virusi vya Corona katika muda saa 24 zilizopita, kulingana na ripoti ya kila siku iliyotolewa na Wizara ya Afya.

Idadi ya maambukizi nchini Italia imefikia 274,644.
Idadi ya maambukizi nchini Italia imefikia 274,644. Shahzad ABDUL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya maambukizi nchini Italia imefikia 274,644.

Mamlaka imeripoti vifo kumi na moja vilivyohusiana na ugonjwa wa Covid-19 katika muda wa saa 24 izilizopita dhidi ya kumi siku moja kabla, na kufikisha jumla ya vifo 35,518 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Italia.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwezi Desemba 2019.

Hivi karibuni shirika la afya Duniani, WHO, lilizitaka nchi zote kutilia mkazo hatua za kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona na kuonya kuwa licha ya jitihada zinazofanyika kutafuta chanjo na dawa ya kupambana na janga la virusi vya Corona, huenda kusiwe na suluhu ya muda mrefu ya kukabiliana na janga hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.