Pata taarifa kuu
ITALIA-UFARANSA-MAREKANi-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya vifo yapungua Italia, Ufaransa na New York

Idadi ya vifo vinavyohusishwa na virusi vya Corona nchini Italia, Ufaransa na Jimbo la New York Marekani ,imeanza kupungua, hata kama bado kunaripotiwa visa kadhaa vya maambukizi katika nchi hizo.

Duka la ukumbusho lilifungwa huko Roma Machi 28, 2020, Italia ikichukua hatua za kuzuia kuenea kwa Covid-19.
Duka la ukumbusho lilifungwa huko Roma Machi 28, 2020, Italia ikichukua hatua za kuzuia kuenea kwa Covid-19. REUTERS/Alberto Lingria
Matangazo ya kibiashara

Italia pekee ,nchi iliyokuwa inaongoza na idadi kubwa ya vifo ulimwengu kwa majuma yaliyopita,iliripoti visa 431 katika saa 24 zilizopita, hii ikiwa ni idadi ya chini kabisa ikilinganiswa na vifo 619 vilivyotokezea siku Jumamosi.

Kiwango cha maambukizi mapya yaliyothibitishwa pia kimeshuka kutoka 4,694 siku ya Jumamosi hadi 4,092 jana Jumapili.

Italia ni ya pili kwa vifo duniani, ikitanguliwa na Marekani, kwa kupoteza watu 19,899 hadi jioni Jumapili.

Hata hivyo, bado inasalia kuwa moja ya mataifa yaliyoathirika sana na Ugonjwa hatari wa Covid-19 ambao Umoja wa Mataifa uliotaja kuwa ni janag la kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.