Pata taarifa kuu

Coronavirus: WHO kutoa ripoti yake kuhusu chanjo ya AstraZeneca Ijumaa

Kamati ya Wataalam wa Shirika la Afya Duniani (WHO) juu ya usalama wa Chanjo itatoa ripoti yake ya mwisho juu ya chanjo dhidi ya COVID-19 ya AstraZeneca Ijumaa wiki hii, msemaji wa shirika hilo amesema.

Mkurugenzi wa WHO katika ukanda wa Ulaya Hans Kluge amesema kwamba faida za chanjo ya AstraZeneca huzidi hatari yoyote na kwamba nchi za Ulaya ambazo zimesitisha matumizi ya chanjo ya AstraZeneca zinapaswa kuanza tena kampeni ya kuchoma sindano ili kuokoa maisha ya raia.
Mkurugenzi wa WHO katika ukanda wa Ulaya Hans Kluge amesema kwamba faida za chanjo ya AstraZeneca huzidi hatari yoyote na kwamba nchi za Ulaya ambazo zimesitisha matumizi ya chanjo ya AstraZeneca zinapaswa kuanza tena kampeni ya kuchoma sindano ili kuokoa maisha ya raia. REUTERS - YVES HERMAN
Matangazo ya kibiashara

Chanjo dhidi ya COVID-19 ya AstraZeneca inashukiwa kusababisha madhara makubwa, baadhi ya nchi zimeamua kusitisha kampeni ya kutoa chanjo hiyo kutokana na madai ya kuganda kwa damu, na kuwa chanjo hiyo imesababisha vifo kwa baadhi ya watu.

Kamati hiyo ilichunguza takwimu na ripoti juu ya visa vichache vya kuganda kwa damu vilivyoripotiwa kwa watu ambao walipokea dozi ya chanjo kutoka kwa maabara hiyo inayomilikiwa na Uingereza Sweden, WHO imesema.

Mkurugenzi wa WHO katika ukanda wa Ulaya Hans Kluge amesema leo Alhamisi kwamba faida za chanjo ya AstraZeneca huzidi hatari yoyote na kwamba nchi za Ulaya ambazo zimesitisha matumizi ya ya chanjo ya AstraZeneca zinapaswa kuanza tena kampeni ya kuchoma sindano ili kuokoa maisha ya raia.

Nchi kadhaa katika Umoja wa Ulaya, ikiwa ni pamoja na Ufaransa na Ujerumani, zimeamua kusitisha kampeni ya kutoa chanjo hii hadi hapo itakapotangazwa tena.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.