Pata taarifa kuu
ULAYA

Chanjo ya AstraZeneca yazua kizungumkuti Ulaya

Mataifa kadhaa ya bara la Ulaya, yamesitisha kutoa chanjo ya AstraZeneca kuzuia maambukizi ya Covid-19 kwa watu wake, kwa hofu kuwa, chanjo hiyo inasababisha kuganda kwa damu mwilini.

Chanjo ya AstraZeneca, inatengezwa kwa ushirkiano wa kampuni kutoka Sweden na Uingereza.
Chanjo ya AstraZeneca, inatengezwa kwa ushirkiano wa kampuni kutoka Sweden na Uingereza. REUTERS - DADO RUVIC
Matangazo ya kibiashara

Tume ya kudhibiti madawa barani Ulaya imesema chanjo hiyo ni salama na hakuna ushahidi kuwa inaleta madhara.

Sweden na Latvia yamekuwa mataifa mengine ya bara Ulaya ambayo yamechukua hatua hiyo na kuungana na mataifa mengine kama Ufaransa, Ujerumani, Hispania na nyingine ambazo zimechukua hatua hiyo.

Shirika la afya duniani WHO limekuwa likisema chanjo hiyo ni salama na inaendelee kutumiwa kwa sababu hakuna ushahidi mpaka sasa kuwa inasababisha madhara.

Hata hivyo, maafisa wa WHO walikutana siku ya Jumanne, kutathmini zaidi usalama wa chanjo hiyo ambapo mamilioni ya watu kote duniani, tayari wameshapata chanjo hiyo.

Nchini Marekani na barani Ulaya, kufikia Jumanne wiki hii, tayari watu Milioni 17 wamepokea chanjo hiyo, huku kukiwa na visa chini ya 40 vya watu kulalamikia damu kuganda baada ya kupata chanjo hiyo.

Chanjo ya AstraZeneca, inatengezwa kwa ushirkiano wa kampuni kutoka Sweden na Uingereza na wakati huu uchunguzi ukiendelea kuhusu visa hivyo, watalaam wa chanjo hii wanasema madhara yanayoweza kujitokeza sio makubwa, ikilinganishwa na uwezo mkubwa wa chanjo hiyo kuzuia maambukizi ya Covid-19.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.