Pata taarifa kuu
UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Zaidi ya kesi mpya 13,300 zathibitishwa nchini Ujerumani

Idadi ya kesi zilizothibitishwa za maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani imeongezeka hadi 671,868, baada ya visa vipya 13,363 kuripotiwa siku iliyopita, kulingana na takwimu zilizotolewa Jumatatu na kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa cha Robert Koch (RKI).

Idadi ya visa vya virusi vya Corona nchini Ujerumani imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni, na katika siku kadhaa zilizopita maambukizi ya kila siku yalipindukia visa 1,000.
Idadi ya visa vya virusi vya Corona nchini Ujerumani imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni, na katika siku kadhaa zilizopita maambukizi ya kila siku yalipindukia visa 1,000. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Taasisi hiyo pia imeripoti vifo vipya 63, na kufanya idadi ya vifo kufikia 11,352 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.

Ulaya inaendelea kukabiliwa na maambukizi mapya kufuaia mlipuko mpya wa COVID-19. Nchi kadhaa barani Ulaya zimerejesha upya hatua kadhaa zilizochukuliwa wakati wa mlipuko wa kwanza, tangu ugionjwa huo kuzuka huko Wuhan, mwichoni mwa mwezi Desemba mwaka jana nchini China.

Wiki iliyopita shirika la Afya Dunia, WHO, limeonya juu ya mlipuko wa janga hatari katika bara la Ulaya.

Bara la Ulaya sasa lina zaidi ya visa vya milioni 12 vya maambukizi ya virusi vya Corona kwa vifo zaidi ya 300,000, ikiwa ni pamoja na Urusi. Shirika la Afya Duniani, WHO, lilionya kuwa wiki chache zijazo hali itakuwa ngumu zaidi.

WHO inasisitiza uvaaji wa barakoa na inatoa wito kwa shule kufunguliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.