Pata taarifa kuu
UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Ujerumani yarekodi visa vipya zaidi 12,000

Idadi ya kesi zilizothibitishwa za maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani imepanda hadi 545,027, baada ya kesi mpya 12,097 kuthibitishwa, kulingana na takwimu zilizotolewa Jumatatu na kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa cha Robert Koch (RKI).

Vifo zaidi ya arobaini na tisa vimeripotiwa, na kufikisha jumla ya vifo 10,530 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.
Vifo zaidi ya arobaini na tisa vimeripotiwa, na kufikisha jumla ya vifo 10,530 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Vifo zaidi ya arobaini na tisa vimeripotiwa, na kufikisha jumla ya vifo 10,530 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini.

Hayo yanajiri wakati mlipuko mpya wa COVID-19 unaendelea kuzusha taharuki barani Ulaya.

Hali ya wasiwasi imeongezeka miongoni mwa wakaazi wa mataifa mengi barani Ulaya kutokana na kurejea tena kwa vizuizi vikali vya kukabiliana na maambukizi pamoja na vifo vya COVID-19.

Wakati huo huo Ufaransa imesema itapiga marufuku uuzwaji wa bidhaa ambazo haziihitajiki sana katika maduka makubwa nchini humo kuanzia kesho, kama mojawapo ya njia ya kukabiliana na janga la Corona.

Ufaransa imetangaza makataa mapya kwa nchi nzima ya watu kutotembea baada ya kuzuka kwa mlipuko wa pili wa virusi hivyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.