Pata taarifa kuu
UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Zaidi ya kesi mpya 18,000 zaripotiwa nchini Ujerumani

Idadi ya visa vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani imepanda hadi 499,694, baada ya visa vipya 18,681 kuthibitishwa siku moja iliyopita, kulingana na takwimu zilizotolewa leo Ijumaa na kituo cah kuzuia na kudhibiti magonjwa cha Robert Koch (RKI).

Idadi ya visa vya virusi vya Corona nchini Ujerumani imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni.
Idadi ya visa vya virusi vya Corona nchini Ujerumani imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni. Ina FASSBENDER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Vifo vipya sabini na saba vimethibitishwa, na kufanya jumla kufikia 10,349 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.

Ongezeko la visa vya maambukizi ya kila siku limeendelea kushuhudiwa katika nchi kadhaa za bara la Ulaya.

Wiki hii Tume ya Ulaya imependekeza mfululizo wa hatua mpya dhidi ya janga la COVID-19 katika bara la Ulaya kutokana na ongezeko la maambukizi mapya, ukitolea wito nchi 27 wanachama wa Umoja huo kuboresha uratibu wao.

Tume ya Ulaya imeshauri serikali kuratibu mikakati yao ya upimaji na kutumia zaidi upimaji maalumu hata kama mfumo wa aina hiyo unaonyesha dalili za mvutano.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.