Pata taarifa kuu
UJERUMANI-CORONA-AFYA-UCHUMI

Coronavirus: Ujerumani kufungua biashara zote Mei 11

Marais wa majimbo (Länder) nchini Ujerumani wanatarajia kukubaliana katika mazungumzo ya simu na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel Jumatano wiki hii kuhusu kuanza kulegeza vizuizi vilivyowekwa kama sehemu ya mapambano dhidi ya Corona.

Vinyozi wamerejea kufanya kazi yao ya kawaida nchini Ujerumani, kama hapa Cologne, Jumatatu, Mei 4, 2020.
Vinyozi wamerejea kufanya kazi yao ya kawaida nchini Ujerumani, kama hapa Cologne, Jumatatu, Mei 4, 2020. REUTERS/Thilo Schmuelgen
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, likinukuu vyanzo viwili vilivyo karibu ya kesi hiyo, Mamlaka katika majimbo hayo zinatarajiwa kutoa idhni ya kufungua tena maduka katika majimbo yote ya Ujerumani, labda kuanzia Mei 11, vyanzo hivyo vimesema. Biashara ndogo ndogo tayari zimeruhusiwa kufunguliwa tena kwa masharti ya kuheshimu hatua za kutokaribiana.

Wakati huo huo, mamlaka inatarajia kupitisha uamuzi wa kuanzishwa tena kwa michuano ya ligi kuu ya soka, Bundesliga, vyanzo hivyo vimeongeza, na kubaini kwamba mechi hizo zitapigwa bila mtu yoyote kuhudhuria.

Michezo kwa wasio wachezaji na watoto pia itafunguliwa tena.

Chanzo kimoja kimesema kwamba mamlaka pia wana nia ya "kufunguwa tena shule za chekechea kusaidia wazazi wengi wanaofanya kazi.

Ujerumani ilifikia hatua mpya Jumatatu wiki hii ya kuanza kulegeza vizuizi ikiwa ni pamoja na kufungua tena majumba ya makumbusho na sehemu za ibada na viwanda kadhaa vya magari, lakini wanasiasa wamegawanyika kuhusu hatua hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.