Pata taarifa kuu
AUSTRALIA-KANISA-HAKI

Australia: Kardinali George Pell ahukumiwa miaka 6 jela

Kardinali wa Australia George Pell, mshauri wa zamani wa Papa Francis na muweka hazina wa zamani wa Vatican, amehukumiwa miaka sita jela na mahakama ya Melbourne baada ya kupatikana mwezi uliopita na hatia ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watoto mwishoni mwa mwaka 1990.

George Pell, mwaka 2017 Melbourne.
George Pell, mwaka 2017 Melbourne. REUTERS/Mark Dadswell/File Photo
Matangazo ya kibiashara

George Pell, mwenye umri wa miaka 77, ni afisa wa ngazi ya juu wa kanisa Katoliki ambaye amepatikana na hatia ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watoto. Anakabiliwa na kifungo cha miaka 50 jela.

"Najua kwamba kwa hukumu hii ya kifungo (...), kuna uwezekano usiishi kwa muda mrefu baada ya kutumikia kifungo chako," Jaji Peter Kidd amesema wakati kesi hiyo ilikuwa ikisikilizwa.

"Kwa mtazamo wangu, mwenendo wako haufai kwa maadili" ya kiongozi wa ngazi ya juu katika kanisa.

George Pell alipatikana na hatia ya unyanyasaji wa kijinsia aliofanya mwishoni mwa mwaka 1990 dhidi ya watoto wawili waliokuwa na umri wa miaka 13 kutoka Kanisa la St Patrick's huko Melbourne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.