Pata taarifa kuu
UFARANSA-USALAMA

Emmanuel Macron kuhusu kesi ya Benalla: "mhusika pekee ni mimi"

Baada ya kukosolewa kuhusu ukimya wake katika kesi ya mshirika wake wa karibu katika masuala ya usalama, Alexandre Benalla, aliyepiga waandamanaji siku ya siku kuu ya Mei mosi, hatimaye rais wa Ufaransa amejitetea akisema kuwa 'mhusika pekee' ni yeye.

Rais Emmanuel Macron, hapa ilikua Julai 17, 2018 huko Paris.
Rais Emmanuel Macron, hapa ilikua Julai 17, 2018 huko Paris. GONZALO FUENTES / POOL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Upinzani umekua ukimtaka azungumze kuhusu mkasa unaomkabili msaidizi wake wa maswala ya Usalama Alexandre Benalla pamoja na muundo wa Ikulu ya Elysee.

Emmanuel Macron alizungumza Jumanne hii Julai 24 mbele ya wajumbe waliochaguliwa kutoka LREM-MoDem na wajumbe kadhaa wa serikali waliokusanyika katika Jengo moja huko Paris, nchini Ufaransa. Karibu wiki moja baada ya kuzuka kwa kesi ya Benalla, Emmanuel Macron alikuja kuwapa moyo wafuasi wa kambi yake, bila hata hivyo kuwepo vyombo vya habari.

Kulingana na taarifa zilizoripotiwa na wabunge waliohudhuria mkutano huo, Emmanuel Macron alisema anaelewa "mkasa uliotokea Mei 1" wa Alexandre Benalla kama "usaliti".

Mapema Jumanne, mbele ya Bunge la Taifa, Mkuu wa Baraza la Mawaziri Patrick Strzoda na Waziri Mkuu Edouard Philippe walimshtumu Benalla, wakati ambapo saa chache baadaye rais Macron alidai kuwa yeye ndiye anahusika. "Huwezi kuwa kiongozi wakati hali ya nchi iko sawa na kujivua uongozi wakati hali inakua ngumu. Ikiwa wanataka muhusika, huyu hapa mbele yenu. Waje kumtafuta. Ninawajibu wananchi wa Ufaransa, " Emmanuela Macron alisema, bila kujua aliyekua akilenga.

"Ikiwa wanatafuta mhusika, ni mimi pekee hakuna mwengine. Nilimwamini Alexandre Benalla. Ni mimi ambaye nilithibitisha adhabu, "ameongeza rais Macron, kulingana na ripoti. Mbele ya tume ya Sheria ya bunge Jumanne mchana wiki hii, Patrick Strzoda alisema kuwa amechukua uamuzi wa kumsimamisha Alexandre Benalla mwenyewe bila kumtaarifu rais wa Jamhuri ambaye alikua ziarani Australia.

Tangu kuanza kwa mkasa huu alhamisi iliopita, rais Macron amekuwa kimya.

Alexandre Benalla, mshiriki wa karibu wa Emmanuel Macron, alijikuta akiwapiga waandamanaji kando ya CRS wakati wa maandamaano ya siku kuu ya wafanyikazi Mei mosi mwaka huu.

Chanzo cha usalama kimese akuwa awali mlinzi huyo Alexandre Benalla, mwenye umri wa miaka 26, alikua amefunguliwa mashtaka yakiwemo, kuingilia kazi ya Polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.