Pata taarifa kuu
UHISPANIA-SIASA

Hatma ya Mariano Rajoy kujulikana Ijumaa Uhispania

Bunge la Uhispania linatarajia kupiga kura ya kutokua na imani na kiongozi wa serikali Mariano Rajoy siku ya Ijumaa. Bw Rajoy anaona kuwa shinikizo la upinzani limeongezeka baada ya chama cha Popular Party (PP, cha mrengo wa kulia) kujikuta matatani katika kesi ya rushwa.

Waziri mkuu wa uhispania Mariano Rajoy.
Waziri mkuu wa uhispania Mariano Rajoy. REUTERS/Sergio Perez
Matangazo ya kibiashara

Kura ya kutokua na imanani na kiongozi wa serikali ya Uhispania iliyowasilishwa wiki iliyopita na chama cha Kisoshalisti cha PSOE itajadiliwa siku ya Alhamisi wiki hii na kupigiwa kura siku ya Ijumaa wakati ambapo wito wa uchaguzi wa wabunge wa mapema ukiendelea.

Ili kuiangusha serikali, upinzani unahitaji kwa uchache kura 176 bungeni. Jambo ambalo ilishindwa kufanikisha katika kura nyingine ya kutokua na imani na kiongozi wa serikali mnamo mwezi Juni mwaka jana.

Chama cha mrengo wa kati cha Ciudadanos (Wananchi), kilisema siku ya Jumamosi kuwa kiko tayari kushirikiana na chama chama cha PSOE kuunga mkono mgombea huru atakayechukua nafasi ya Mariano Rajoy, ambaye serikali tayari inakabiliwa na udhaifu kutokana na mgogoro wa Catalonia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.