Pata taarifa kuu
UHISPANIA

Waziri mkuu wa Uhispania kukutana na baraza lake kuhusu Catalonia

Waziri mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy leo Jumamosi anakutana na baraza lake la mawaziri kupanga mipango ya kuchukua mamlaka kutoka katika jimbo la Catalonia ikiwa kiongozi wa eneo hilo hatasitisha mchakato wa kujitenga.

Mariano Rajoy,Waziri mkuu wa Uhispania
Mariano Rajoy,Waziri mkuu wa Uhispania MIGUEL RIOPA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya hapo jana Mfalme wa Uhispania Felipe VI ,kukosoa kile alichosema kuwa "jaribio lisilokubalika la kujitenga" la Catalonia huku serikali na kuongeza kwamba mgogoro uliotokana na kura ya kujitenga iliyopigwa marufuku Oktoba 1 lazima utatuliwe kwa njia ya taasisi halali za kidemokrasia

Madrid inanufaika na mamlaka ya kikatiba katika kudhibiti uasi wa majimbo katika mojawapo ya mataifa ya Ulimwengu wa Magharibi, lakini haijawahi kutumia mamlaka hayo.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wameunga mkono Madrid huku mkuu wa bunge la Umoja wa Ulaya Antonio Tajani akionya kuwa jaribio la kurekebisha mipaka ya Ulaya mara nyingi "limesababisha fujo mbaya.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.