Pata taarifa kuu
CATALONIA-UHISPANIA-HAKI

Rais wa Catalonia kutekeleza matokeo ya kura ya maoni

Rais wa Catalonia Carles Puigdemont alihutubia wakazi wa eneo hilo siku ya Jumatano, ambapo alifutilia mbali shutma za Mfalme wa Uhispania Felipe VI. Bw. Puigdemont alimkosoa Mfalme Felipe VI kwa kutotambua matakwa ya wakazi wa Catalonia.

Rais wa Catalonia, Carles Puigdemont.
Rais wa Catalonia, Carles Puigdemont. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo kiongozi huyo hajatamka neneo la uhuru,lakini alithibitisha nia yake ya kutekeleza matokeo ya kura ya maoni iliyopigwa siku ya Jumapili Oktoba 1. Alisema wako tayari kuketi kwenye meza ya mazungumzo.

Katika hotuba yake ya Oktoba 4, Carles Puigdemont alishutumu mfalme wa Uhispania, ambaye aliwatuhumu viongozi wa Catalonia siku moja kabla kuhatarisha utulivu wa Uhispania nzima. "Mfalme anajikusanyia hotuba na sera za serikali ya [Mariano] Rajoy - ambazo ni hatari kuhusu Catalonia - kwa kupuuzia kwa makusudi matakwa ya maelfu ya wakazi wa Catalonia ambao hawafikiri kama wao, ambao ni waathirika wa vurugu za polisi ambazilizolaaniwa na ulimwengu mzima, "Bw Puigdemont alisema.

Madrid yakataa mazungumzo yoyote

Carles Puigdemont amesema "mlango wa mazungumzo uko wazi na kwa heshima ya wengine," licha ya Madrid kupinga jambo hilo. Hoja hiyo imefutiliwa mbali saa chache baadaye na serikali ya Mariano Rajoy. Katika taarifa, Bw. Rajoy alisema: "Kama Bw. Puigdemont anataka majadiliano au mazungumzo, au kutuma wapatanishi, anajua kikamilifu kile atachotakiwa kufanya kabla: kurudi kwenye njia ya sheria, ambayo kamwe hangeliivunja".

Kinyume na hilo rais wa Catalonia alisema wakati wa hotuba yake: "hatuwezi kubabaishwa na yeyote. Serikali yangu haitokwenda kinyume na ahadi za amani, utulivu, lakini pia uimarishaji ambao ndio njia tuliyochagua ".

Ulaya inatiwa wasiwasi na hali hiyo inayojiri nchini Uhispania. Ubelgiji umezitaka pande husika kuketi kwenye meza ya mazungumzo

Kwa mujibu wa matokeo ya kura ya maoni, kura ya ndiyo ilishinda kwa 90% kwa kiwango cha ushiriki uliofikia zaidi ya 42%.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.