Pata taarifa kuu
CATALONIA-UHISPANIA-HAKI

Serikali ya Catalonia yapata haki ya kujitawala

Serikali ya Catalonia imetangaza kwamba imepata ushindi wa kujitawala baada ya wakazi wake kushiriki kwa wingi katika kura ya maoni ya siku ya Jumapili Oktoba 1.

Wanaharakati wanaotaka eneo la Cataloni kujitawala washangilia ushindi wao wa "Ndiyo" kwa Cataloni kujitawala, baada ya kura ya maoni inayochukuliwa na serikali ya Uhispania kuwa ni kinyume cha sheria.
Wanaharakati wanaotaka eneo la Cataloni kujitawala washangilia ushindi wao wa "Ndiyo" kwa Cataloni kujitawala, baada ya kura ya maoni inayochukuliwa na serikali ya Uhispania kuwa ni kinyume cha sheria. REUTERS/Susana Vera
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Catalonia imethibitisha kwamba kura ya "ndiyo" kwa uhuru imeshunda kwa 90%, baada ya kura ya maoni yakujitawala iliyopigwa marufuku na serikali kuu ya Uhispania.

Kura ya maoni ya mwaka 2014 kuhusu kujitawala kwa eneo hilo ilipata ushindi wa 80%, matokeo haya hayashangazi lakini yanaonyesha kuwawakazi wa Catalonia wamekua sasa na muamko wa kujitawala.

Kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Catalonia, watu milioni 2.26 walipiga kura, huku milioni 2.02 walipiga kura ya "ndiyo". Watu 176,000 walipigia kura ya "hapana"kwa jumla ya watu watu milioni 5.3 walioorodheshwa kupiga kura. Kwa mujibu wa mamlaka husika, kiwango cha ushiriki kilifikia 42.3%.

"Siku hii ya leo ya matumaini na mateso, watu wa Catalonia wameshinda haki yao ya kuwa na taifa huru kama jamhuri," Bw Puigdemont alisema alipotoa hotuba kupitia televisheni akiandamana na maafisa wengine wa vyeo vya juu wa Catalonia.

Mahakama ya katiba nchini Uhispania imeitangaza kura hiyo ya maoni kuwa nikinyume na sheria

Mwendendo wa serikali kuu ya Uhispania kuwatuma askari kuondoa masanduku ya kura na kuzuia watu kupiga kura, ilisababisha hali ya sintofahamu katika eneo hilo. Makabiliano kati ya vikosi vya usalama na wapiga kura ulisababisha zaidi watu 800 kujeruhiwa, kwa mujibu wa serikali ya Catalonia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.