Pata taarifa kuu
UFARANSA-KAZI

Edouard Philippe: Mabadiliko katika sekta ya kazi yana malengo mazuri

Serikali ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, imezindua mabadiliko makubwa katika sekta ya kazi nchini humo.

Waziri Mkuu wa Ufaransa Edouard Philippe.
Waziri Mkuu wa Ufaransa Edouard Philippe. REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Edouard Philippe, amesema mabadiliko haya yana malengo mazuri yanayolenga kuimarisha sekta hiyo na kuboresha mazingira ya kazi.

Miongoni mwa sera mpya ni pamoja na kampuni kuwaongezea mshahara wafanyikazi wake kutoka asilimia 20 hadi 25 kila mwaka.

Kiwango cha ukosefu wa ajira nchini Ufaransa ni mara mbili zaidi ikilinganishwa na hali ilivyo katika nchi jirani za Uingereza na Ujerumani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.