Pata taarifa kuu
UJERUMANI-G20-USALAMA

Viongozi wa G20 kukutana Hamburg, Ujerumani

Viongozi kutoka mataifa 20 yanayoongoza kwa uchumi duniani wanaelekea mjini Hamburg kushiriki katika mkutano wa G20.

Wanaharakati wa Oxfam wakijifananisha na Donald Trump, Angela Merkel au Theresa May wakiandamana katika mji wa Hamburg, Julai 6, 2017.
Wanaharakati wa Oxfam wakijifananisha na Donald Trump, Angela Merkel au Theresa May wakiandamana katika mji wa Hamburg, Julai 6, 2017. REUTERS/Fabrizio Bensch
Matangazo ya kibiashara

Usalama umeimarishwa katka mji huo huku wanaharakati wakiandaa maandamano makubwa kesho, kupinga mkutano huo wanaoita wa kibepari.

Hata hivyo, Wakuu wa nchi hizo watakutana kwa siku mbili siku ya Ijumaa na Jumamosi kuzungumzia maswala mbalimbali ya kichumi na kiusalama hasa namna ya kupambana na makundi ya kigaidi kama Islamic State.

Wachambuzi wa siasa za Kimataufa wanasema mkutano huu utafanyika wakati huu viongozi wa mataifa hayo wakitthathmini ikiwa wataendelea kuitegemea Marekani kama kiongozi wake.

Hata hivyo, China inaonekana haiko tayari kutoa uongozi pekee yake lakini inatarajiwa kuwa ikaugana na Urusi pamoja na Ujerumani.

Mbali na masuala ya kiuchumi na usalama, utekelezwaji wa mkataba wa kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa, ambao Marekani imejiondoa.

Suala la wimbi la wakimbizi wanaokimbilia barani Ulaya litajadiliwa bila kusahau majaribio ya mara kwa mara ya makombora yanayotekelezwa na Korea Kaskzini.

Rais wa Marekani Donald Trump, rais wa Ufaransa Francois Hollande, rais wa China Xi Jping, ni miongoni mwa viongozi watakaohudhuria mkutano huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.