Pata taarifa kuu
UFARANSA-LE PEN-HAKI

Kesi ya wasaidizi wa Bunge la Ulaya: Marine Le Pen achunguzwa

Kiongozi wa chama cha Front National Marine Le Pen aalichunguzwa siku ya Ijumaa, Juni 30, wakili wake alitangaza. Alishtakiwa kwa kuvunja uaminifu katika uchunguzi wa wasaidizi wa Bunge la Ulaya. 

Marine Le Pen, Januari 17, 2017 kwenye Bunge la Ulaya mjini Strasbourg.
Marine Le Pen, Januari 17, 2017 kwenye Bunge la Ulaya mjini Strasbourg. REUTERS/Christian Hartmann/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Marine Le Pen aliripoti kwenye Mahakama Kuu ya Paris siku ya Ijumaa mchana, na kuanza kuhojiwa kuhusu kuvunja uaminifu kama mbunge wa Bunge la Ulaya kati ya mwaka 2009 na 2016 kwa matumizi ya fedha la Bunge la Ulaya kwa niaba ya Bii Griset na Bw. Legier, wasaidizi wawili wa bunge katika kesi hiyo, chanzo mahakama kimearifu.

"Kulingana na ahadi zake alizotoa wakati wa kampeni za urais, Marine Le Pen aliripoti siku ya Ijumaa kwenye Mahakam Kuu ya Paris baada ya majaji wa mahakama hiyo kumtaka afanye hivo," alisema wakili wake, Rodolphe Bosselut, na kuongeza kwamba atakata rufaa siku ya Jumatatu dhidi ya uchunguzi huo ambao, akibaini kwa unakiuka kanuni ya mgawanyo wa madaraka.

Hadi sasa,kiongozi wa chama cha Front National alikataa kukutana na majaji Mbunge huyo mpya wa eneo la Pas-de-Calais aliweka mbele Machi 10 kinga aliokuwa nayo ya ubunge wa Ulaya kwa kukataa hati ya kwanza ya majaji na kusema kuwa yuko tayari kujibu maombi yao baada ya uchaguzi wa urais na wa wabunge.

Majaji wanatafuta kujua kama chama chama cha mrengo wa kulia kilianzisha mfumo wa jumla wa kulipa maafisa wake kwa fedha za Bunge la Ulaya, na kuwalipa mishahara kama wasaidizi wa wabunge wake wa Ulaya, bila hata hivyo kazi yaokuwa na uhusiano na shughuli za Bunge la Ulaya.

Marine Le Pen ni mmoja wa wabunge 17 kutoka chama cha FN, ikiwa ni pamoja na baba yake Jean-Marie Le Pen, na rafiki yake Louis Aliot, wanalengwa na uchunguzi huo uliofunguliwa nchini Ufaransa mwaka 2015, unaowahusisha wasaidizi arobaini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.