Pata taarifa kuu
UINGEREZA-UGAIDI

Mauaji ya kigaidi London watu sita wafariki dunia

Watu sita wamefariki dunia na wengine kadha kujeruhiwa katika tukio linalotajwa kuwa la kigaidi katikati mwa jiji la London ambapo washambuliaji watatu waliuawa kwa risasi polisi wameeleza.

Hali ya taharuki ilitanda katika eneo la daraja la London
Hali ya taharuki ilitanda katika eneo la daraja la London REUTERS/Hannah McKay
Matangazo ya kibiashara

Shambulizi hilo lilihusisha watu kugongwa na gari na wengine kuchomwa visu katika eneo la Daraja la London.

Kwa mujibu wa polisi washambuliaji walikutwa wamevalia fulana za kujitolea muhanga zisizofanya kazi.

Viongozi mbalimbali wa mataifa wamelaani tukio hilo na kutuma salamu za pole na kuonesha mshikamano na taifa la Uingereza ambapo raisi wa Marekani Donald Trump ameahidi taifa lake kutoa msaada wowote utakao hitajika kukabiliana na ugaidi nchini Uingereza.

Kwa upande wake raisi wa Ufaransa Emanuel Macron amesema taifa lake linashikamana na Uingereza katika kukabiliana na matukio haya ya kigaidi.

Tukio hilo linatekelezwa majuma kadhaa tu baada ya watu 22 kuuliwa katika shambulio la kujitoa muhanga, ndani ya uwanja mmoja wa burudani huko mjini Manchester.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.