Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHAGUZI

Macron ashutumu shambulizi la kimtandao dhidi yake

Timu ya kampeni ya mgombea urais nchini Ufaransa Emmanuel Macron imeshutumu shambulizikubwa la kimatandao dhidi ya kampeni zake baada ya nyaraka nyingi za ndani kuonekana mtandaoni jana usiku, karibu saa 24 kabla ya uchaguzi.

Mgombea urais nchini Ufaransa Emmanuel Macron
Mgombea urais nchini Ufaransa Emmanuel Macron
Matangazo ya kibiashara

Wafanyakazi wa mgombea huyo mwenye msimamo wa wastani wamegadhabishwa na hatua hiyo ambapo wamesema kutolewa kwa maelfu ya barua pepe, nyaraka za uhasibu na faili nyingine ni jaribio la kuvuruga demokrasia,kama lile lililoshuhudiwa wakati wa kampeni za mwisho za urais nchini Marekani

Nyaraka hizo zimeenea kwenye mitandao ya kijamii kabla ya usiku wa manane jan Ijumaa baada ya Macron na mpinzani wake Marine Le Pen kuhitimisha rasmi kampeni zao kwa ajili ya uchaguzi wa duru ya pili kesho Jumapili.

Timu ya Macron imesema nyaraka hizo ziliibiwa juma lililopita wakati viongozi kadhaa kutoka chama chake cha En Marche kubaini kuvamiwa kwa barua pepe zao binafsi na za kazi, moja ya mashambulizi makubwa na ya mara kwa mara ya kimtandao dhidi ya Macron tangu uzinduzi wa kampeni.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.