Pata taarifa kuu
UFARANSA-AJALI-MAUAJI

Ufaransa yatangaza maombolezo ya kitaifa ya siku tatu

Serikali ya Ufaransa imetangaza maombolezo ya kitaiafa kuanzia Jumamosi hadi Jumatatu ya wiki ijayo, baada ya lori lililoingizwa kwa kasi Alhamisi Julai 14 usiku katika umati wa watu waliokua wakitazama urushwaji wa fataki katika sherehe ya maadhimisho ya Siku kuu ya kitaifa ya Julai 14.

Madaktari wakiondoa miili ya watu waliopoteza maisha katika eneo la Promenade des Anglais baada ya lori kuingizwa kwa kasi katika umati wa watu waliokua wakisherehekea maadhimisho ya Julai 14, Nice Julai 15, 2016.
Madaktari wakiondoa miili ya watu waliopoteza maisha katika eneo la Promenade des Anglais baada ya lori kuingizwa kwa kasi katika umati wa watu waliokua wakisherehekea maadhimisho ya Julai 14, Nice Julai 15, 2016. AFP/BORIS HORVAT
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lililotokea katika eneo la Promenade des Anglais mjini Nice liliwaua watu 84, wengine kadhaa kujeruhiwa, na watu wengine 18 wakiwa katika "hali mbaya" kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya ndani Bernard Cazeneuve. Rais Hollande amezungumzia "mashambulizi hayo kuwa ni ya kigaidi bila shaka”.

Mwendesha mashitaka wa mjini Paris François Molins katika mkutano na vyombo vya habari mjini Nice, Julai 15, 2016.
Mwendesha mashitaka wa mjini Paris François Molins katika mkutano na vyombo vya habari mjini Nice, Julai 15, 2016. GIUSEPPE CACACE / AFP

Mwendesha mashitaka wa mjini Paris, François Molins, katika taarifa yake Ijumaa hii Julai 15 saa 11 jioni, ametoa ripoti ya hivi karibuni kuhusu shambulizi la mjini Nice. “Watu 84 wamepoteza maisha, wakiwemo watoto na vijana 10, majeruhi 202, ikiwa ni pamoja na watu 52 walio katika hali mbaya na 25 katika chumba cha wagonjwa mahututi, “ amesema François Molins.

Baada ya shambulizi hilo la mjini Nice, Rais François Hollande amelihutubia taifa Ijumaa hii katika Ikulu kimkoa ya mji wa Nice kusini mwa Ufaransa. Rais Hollande aliyekuja "kushikamana" na "kuungana" na Serikali, ameeleza kwamba Ufaransa bado inakabiliwa na vitendo vya kigaidi. "Bado tunakabiliwa na tishio," amesisitiza François Hollande.

"Wakati huu ambapo ninazungumza, watu 80 wameuawa, watu 84 hasa, na watu zaidi ya hamsini bado wako katika hali mbayakabisa, ninamaanisha, kati ya maisha na kifo ...", amesema Rais Hollande

Mataifa mbalimbali duniani yaungana na Ufaransa

Nchini Marekani, viongozi mbalimbali serikalini wameelezea mshikamano wao na Paris katika tukio hilo. Barack Obama amelaani vikali, "kile kinachoonekana kuwa shambulio la kutisha nchini Ufaransa."

Mgombea urais katika chama cha Republican, Donald Trump, amefuta mara moja mkutano wake na waandishi wa habari uliyokua umepangwa kufanyikaIjumaa hii.

Waziri Mkuu wa Canada alionyesha kwa upande wake toka Alhamisi hii jioni mshikamano wake na Ufaransa. "Canada inahuzunishwa na shambulizi (Alhamisi) hii jioni njini Nice," alisema Justin Trudeau kwenye akaunti yake Twitter.

Nichini Brazil Kaimu Rais, Michel Temer, amelaani kitendo hiki kiliyoendeshwa "dhidi ya raia wasiokuwa na hatia waliokua wakiadhimisha maadili ya juu kwa wote, uhuru wa watu, usawa kati ya wananchi na udugu."

"Ujerumani iko bega kwa bega na Ufaransa katika mapambano dhidi ya ugaidi," amesema Kansela wa Ujerumani Angela Merkel Ijumaa hii Julai 15 asubuhi. "Kauli yangu inatosha tu kusema tunaungana na marafiki zetu wa Ufaransa," ameongeza Angela Merkel.

"Urusi inashikamana na raia wa Ufaransa katika siku hii ngumu," amesema Rais wa Urusi Vladimir Putin. "Urusi uko tayari kwa ajili ya ushirikiano wa karibu na Ufaransa katika mapambano dhidi ya ugaidi."

Waziri Mkuu wa Uturuki Binal Yildirim ameandika kwa Kifaransa kwenye ukurasa wake wa Twitter: "Uturuki, daima inashirikiana na mataifa duniani katika mapambano ya kimataifa dhidi ya ugaidi, na inaungana naUfaransa katika siku hii ngumu."

Marais mbalimbali kutoka nchi za Afrika vile vile wameonyesha hisia zao baada yatukio hilo la kuhuzunisha lililotokea nchini Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.