Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-COX

Polisi ya Uingereza yatangaza kifo cha Mbunge Jo Cox

Polisi ya Uingereza imetangaza Alhamisi hii mchana, kifo cha Mbunge Jo Cox, aliyeshambuliwa siku hiyo hiyo kaskazini mwa Uingereza.

Askari polisi wa Uingereza akisimama na eneo alikoshambuliwa  Jo Cox, Birstall, karibu na Leeds, Juni 16, 2016.
Askari polisi wa Uingereza akisimama na eneo alikoshambuliwa Jo Cox, Birstall, karibu na Leeds, Juni 16, 2016. REUTERS/Craig Brough
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uingereza, Jo Cox alikua alijeruhiwa na risasi na baadae kupigwa kisu na mtu mweny umi wa miaka 52.

Kufuatia kisa hiki cha kushambuliwa kwa Mbunge huyo, kambi inayounga mkono Uingereza kubaki katika Umoja wa Ulaya ilitangaza mapema Alhamisi mchana kwamba inasimamisha kampeni zake dhidi ya nchi hiyo kuondoka katika Umoja wa Ulaya.

Jo Cox, Mbunge kutoka Uingereza, mwenye umri wa miaka 41, alikua anaunga mkono Uingereza kubaki katika Umoja wa Ulaya. Alijeruhiwa kwa risasi wakati alipokua akikutana na wafuasi wake katika jimbo lake. Baada ya kupigwa risasi, Jo Cox alidondoka kati ya magari mawili madogo madogo, mmoja wa mashahidi amesema.
Jo Cox aliingilia kati wakati watu wawili walikua wakipigana. Jo Cox alisafirishwa hospitali akiwa katika hali mbaya, kaskazini mwa nchi.

Shambulizi hili limetokea wiki moja kabla ya kura ya maoni juu kuondoka au la kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya. Kufuatia kitendo hicho, kampeni dhidi ya kuondoka kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya imesimamishwa. Kwenye Twitter, David Cameron, Waziri Mkuu wa Uingereza, amesema anatiwa "wasiwasi", akiongeza kuwa "katika mawazo yetu na sala zetu tuko pamoja na Jo na familia yake."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.