Pata taarifa kuu
UINGEREZA-UE

Kambi inayotaka Uingereza kujiondoa katika EU yaongoza

Siku tisa kabla ya kura ya maoni ya Juni 23, tafiti tatu zinaonyesha leo Jumanne kuwa kambi inayotaka Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya inaongoza kwa alama saba dhidi ya wafuasi wanaotaka nchi hiyo kubaki katika umoja huo.

Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, akiambatana na Mkuu wa jiji la London Sadiq Khan, katika mji mkuu wa Uingereza, ili kutetea kubaki kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya.
Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, akiambatana na Mkuu wa jiji la London Sadiq Khan, katika mji mkuu wa Uingereza, ili kutetea kubaki kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya. REUTERS/Yui Mok/Pool
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo kichwa cha habari kwenye gazeti la Sun kinatolea wito wasomaji wake kupiga kura ya Uingereza kujiondoka katika Umoja wa Ulaya.

Utafiti unaojulikana kama YouGov uliyoendeshwa na gazeti la Times linaipa kambi inayotaka Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya 46% ya kura dhidi ya 39% ya kambi inayotaka Uingereza kubaki katika Umoja huo. 4% ya kura iliyobaki, wanasema ni raia ambao hawatopiga kura. Wiki moja iliyopita, utafiti wa gazeti wa Times / YouGov uliwapa wafuasi wanaotaka Uingereza kubaki katika Umoja wa Ulaya kura nyingi dhidi ya kambi ya wafuasi wanaotaka nchi hiyo kujiondoa katika Umoja wa Ulaya.

Uchaguzi unaojulikana kama ICM wa gazeti la Guardian unaipa kambi inayotaka Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya 53% ya kura katika dhidi ya 47% ya kambi inayotaka nchi hiyo kutojiondoa katika Umoja wa Ulaya. Wiki mbili zilizopita, kambi hizi zilikaribiana (52% - 48%).

Hatimaye, uchunguzi unaojulikana kama ORB wa gazeti la Daily Telegraph unaipa kambi inayotaka uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya 49% ya kura dhidi ya 48% ya kura ya kambi inayotaka nchi hiyo kubaki katika Umoja wa Ulaya.

Kambi inayotaka Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya pia imepata msaada kutoka gazeti la Sun, ambalo limechapisha maneno kama "BELEAVE in britain" (maneno yanayoonyesha Uingereza kuwa tayari kujiondoa katika Umoja wa Ulaya).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.