Pata taarifa kuu
G7-UINGEREZA-UCHUMI

G7 yaisihi Uingereza kutojoundoa katika EU

Viongozi wa mataifa yaliyoendelea kiwanda duniania ya G7 wameafikiana kwa pamoja kuunga mkono Uingereza kutojiondoa katika Umoja wa Ulaya EU.

Viongozi wa G7 katika mkutano wao wa kwanza wa kikazi katika kasri la Elmau, Bavaria, Juni 7, 2015.
Viongozi wa G7 katika mkutano wao wa kwanza wa kikazi katika kasri la Elmau, Bavaria, Juni 7, 2015. REUTERS/Alain Jocard/Pool
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wanaokutana nchini Japan wamesema kuondoka kwa Uingereza katika umoja huo kutayumbisha uchumi wa dunia.

Wananchi wa Uingereza tarehe 23 mwezi ujao watapiga kura, kuamua ikiwa wanataka kuendelea kuwa katika Umoja huo au kuondoka.

Waziri Mkuu David Cameron amekuwa akifanya kampeni kuwahimiza Waingereza kupiga kura ya kusalia katika umoja huo.

Mbali na suala la Uingereza, viongozi hao wamezungunzia maswala mengine kama ugaidi, uchumi na suala la wakimbizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.