Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-COX

Mbunge mmoja ajeruhiwa vibaya Uingereza

Mbunge mmoja anayetetea Uingereza kubaki katika Umoja wa Ulaya nchini Uingereza, Jo Cox amejeruhiwa kwa risasi Alhamisi hii, huku akichomwa kisu na mshambuliaji mwenye umri wa miaka 52.

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na Rais wa Tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker mjini Brussels, Februari 16, 2016.
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron na Rais wa Tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker mjini Brussels, Februari 16, 2016. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Kampeni dhidi ya kuondoka au la kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya imesimamishwa baada ya tukio hilo.

Jo Cox, Mbunge kutoka Uingereza, mwenye umri wa miaka 41, anaunga mkono Uingereza kubaki katika Umoja wa Ulaya. Amejeruhiwa kwa risasi wakati alipokua akikutana na wafuasi wake katika jimbo lake. Baada ya kupigwa risasi, Jo Cox alidondoka kati ya magari mawili madogo madogo, mmoja wa mashahidi amesema.

Jo Cox aliingilia kati wakati watu wawili walikua wakipigana. Jo Cox alisafirishwa hospitali akiwa katika hali mbaya, kaskazini mwa nchi. Mtu mwingine alipata majeraha madogo.

Waziri Mkuu "atiwa wasiwasi"

Shambulizi hili limetokea wiki moja kabla ya kura ya maoni juu kuondoka au la kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya. Kufuatia kitendo hicho, kampeni dhidi ya kuondoka kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya imesimamishwa. Kwenye Twitter, David Cameron, Waziri Mkuu wa Uingereza, amesema anatiwa "wasiwasi", akiongeza kuwa "katika mawazo yetu na sala zetu tuko pamoja na Jo na familia yake."

Kiongozi wa chama cha Labour, Jeremy Corbin amesema "anahuzunishwa na kisa hicho."

Jo Cox, aliyechaguliwa tangu mwaka 2015, anaolewa na Breendan Cox, mshauri wa zamani wa Gordon Brown, Waziri Mkuu wa zamani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.