Uturuki yamuitisha balozi wake Ujerumani
Uturuki imemuitisha balaozi wake nchini Ujerumani kutokana na uamuzi wa Bunge la Ujerumani kupitisha Alhamisi hii azimio linalotambua mauaji ya kimbari ya Waarmenia.
Imechapishwa:
Ujerumani inabaini kwamba mauaji hayo yalitekelezwa na utawala wa Ottoman. Serikali ya Uturuki imefutilia mbali tuhuma hizo, Waziri Mkuu wa Uturuki, Binali Yildirim, ametangaza.
"Balozi wa Uturuki nchini Ujerumani ameitishwa kwa mashauriano," Bw Yildirim amesema, akinukuliwa na shirika la habari linalounga mkono serikali la ANATOLIA.
Kwa upande wake rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema azimio la Bunge la Ujerumani litaathiri mahusiano ya Uturuki na Ujerumani.