Pata taarifa kuu
EU-UTURUKI-WAHAMIAJI

EU mbioni kuishawishi Uturuki kuzuia wahamiaji

Umoja wa Ulaya unatazamiwa Jumatatu hii mjini Brussels kuishawishi Uturuki kusaidia kudhibiti mgogoro wa wahamiaji ambao unatishia umoja wake wakati huo huo watu 18 wamekufa maji baada ya boti lao kuzama.

Waziri Mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu (kulia) na Rais wa Baraza la Ulaya Donald Tusk (kushoto) wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya mkutano mjini Ankara Machi 3, 2016.
Waziri Mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu (kulia) na Rais wa Baraza la Ulaya Donald Tusk (kushoto) wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya mkutano mjini Ankara Machi 3, 2016. AFP
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, Umoja wa Ulaya unasema uko tayari kusaidia Ugiriki, ambayo bado inatarajia kuwapokea wahamiaji 100,000 mwishoni mwa mwezi Machi kutoka nchi jirani ya Uturuki.

Viongozi kutoka nchi 28 wanachama wa Umoja wa Ulaya, Jumatatu hii, watachangia chakula cha mchana pamoja na Waziri Mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu wakati ambapo kuwasili kwa wakimbizi milioni 1.25 wanaoomba hifadhi kumeugawa Umoja wa Ulaya.

Davutoglu atakuwa mjini Brussels siku ya Jumapili usiku kwa "maandalizi ya mkutano" wa faragha pamoja na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte, ambaye nchi yake inashikilia uenyekiti wa Umoja wa Ulaya, kwa mujibu wa vyanzo vya kidiplomasia.

Mkutano huu mpya utafanyika katika hali ya sintofahamu kati ya Umoja wa Ulaya na Uturuki, amayo imeomba kwa muda mrefu kujiunga na umoja huo, huku Umoja wa Ulayaukiwa na hofu ya ukandamizaji dhidi ya vyombo vya habari vinavyompinga Rais Recep Tayyip Erdogan.

Mwishoni mwa mwezi Novemba,Umoja wa Ulaya ulikua ulisaini "mpango wa utekelezaji" na serikali ya Ankara kwa kuwazuia wahamiaji wanaondoka kwa maelfu kutoka pwani ya Uturuki wakielekea katika visiwa vya Ugiriki.

Hayo yakijiri wahamiaji 18 wamekufa maji Jumapili hii baada ya boti lao kuzama kwenye pwani ya kituo cha mapumziko cha Didim (Kusini-Magharibi mwa Uturuki), kwa mujibu wa mamlaka ya Uturuki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.