Pata taarifa kuu
UGIRIKI-MALEDONIA-WAHAMIAJI

Wahamiaji: ghasia katika mpaka wa Ugiriki na Makedonia

Hali ya taharuki imeendelea kutanda Jumatatu hii alaasiri kwenye mpaka wa Ugiriki na Makedonia, baada ya polisi ya Makedonia kurusha mabomu ya machozi dhidi ya mamia ya wahamiaji waliokua wakiwajaribu kuvunja uzio wa mpakani.

Wakimbizi wakikabiliana na Polisi ya Ugiriki kwenye eneo la mpaka wa Ugiriki na Makedonia la Idomeni, Februari 29, 2016.
Wakimbizi wakikabiliana na Polisi ya Ugiriki kwenye eneo la mpaka wa Ugiriki na Makedonia la Idomeni, Februari 29, 2016. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Wahamiaji hao wanapinga dhidi ya kufungwa kwa mipaka, suala ambalo limeugawanya Umoja wa Ulaya.

Wahamiaji na wakimbizi zaidi ya 7,000 wamekua wamezuliwa Jumatatu hii katika eneo la mpakani la Idomeni nchini Ugiriki, baada ya vikwazo viliowekwa na nchi kadhaa ikiwa ni pamoja na Makedonia kuhusu idadi ya watu wanaoruhusiwa kuingia katika ardhi zao.

Wakati ambapo Jumapili hii Makedonia haikumruhusu mhamiaji hata mmoja kuvuka mpaka wake. Hata hivyo Jumatau hii Alfajiri, wakimbizi 300 kutoka Iraq na Syria hatimaye waliweza kuingia Makedonia.

Saa sita mchana, kundi jingine la watu 300 kutoka Iraq na Syria, wakiwemo wanawake na watoto, walijaribu kuvunja sehemu moja ya nyaya za chuma za uzio unaoashiria mpaka na Makedonia. Polisi ya Makedonia wamejibu kwa kurusha mabomu ya machozi ili kushinikiza wahamiaji kupiga hatua kadhaa nyuma na kuwazuia kuingia katika ardhi yao.

Kwa mujibu wa shirika lisilo la kiserikali la Madaktari wa Ulimwengu "Médecins du Monde" (MDM) waliokua eneo hilo, "kwa uchache watu 30 wameomba watibiwe, ikiwa ni pamoja na watoto wengi."

Kwa mujibu wa MDM, idadi ya sasa ya wahamiaji katika eneo la mpakani la Idomeni ni mara nne zaidi ya uwezo wa kambi mbili ziliojengwa karibu na eneo la mpakani, na watu wengi watalazimika kulala katika mashamba.

Abdaljalil, raia wa Syria, mwenye umri wa miaka 22, mkazi wa jimbo la Aleppo, anasema kwamba amekata tamaa. "Hakuna mtu anayetueleza kwa nini hatuwezi kuvuka. Hali ni ngumu hapa, hakuna chakula ama mahali pa kulala (...) na siwezi kurudi Aleppo. "

Makedonia ni nchi ya kwanza kwenye barabara za nchi za Balkan, inayotumiwa na wahamiaji wanaowasili katika visiwa vya Ugiriki wakitokea katika pwani ya za Uturuki na wanataka kuelekea katika nchi za Ulaya ya Kati na Kaskazini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.