Pata taarifa kuu
UGIRIKI - MIPAKA

Ugiriki yapewa makataa na UN kuhusu swala la udhibiti wa mipaka

Wakuu wa nchi za Umoja wa Ulaya wameipa makataa ya miezi mitatu nchi ya Ugiriki kuhakikisha inarekebisha mifumo yake ya udhibiti maeneo ya mipaka ya bahari yake, katika kukabiliana na wimbi la wahamiaji, ama vinginevyo nchi hizo zichukuwe hatua ya kufuta matumizi ya Schengen kwenye mipaka yake yote na nchi hizo.

REUTERS/Darrin Zammit
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu umechukuliwa baada ya mawaziri wa ulinzi kukiri kuwa nchi ya Ugiriki imekuwa kama kisiwa cha wakimbizi wote duniani kupita kwenye nchi hiyo kuingia barani Ulaya, hali ambayo isipodhibitiwa italeta hali tetet kwenye nchi zote za Ulaya.

Wakuu wa Ulaya wanaona kuwa nchi ya ugiriki haifanyi jitihada kukabiliana na wimbi la wahamiaji na badala yake, wahamiaji na wakimbizi wanatumia mwanya huo kuingia ulaya kupitia Ugiriki.

Katika taarifa ya Umoja wa Ulaya, inasema eneo la Schengen linakabiliwa na matatizo makubwa sana, Ugiriki inakabiliwa na mzozo ambao unaouathiri Umoja wa Ulaya na ambayo yanatakiwa kujadiliwa kwa pamoja.

Wimbi kubwa la wakimbizi limekimbilia nchini Ugiriki ambapo Umoja wa Ulaya unaona kwamba Ugiriki inatakiwa kufanya juhudi za ziada ili kudhibiti zaidi hali hiyo.

Uamuzi huo wa leo Ijumaa unatowa nafasi ya matumizi ya kipengele nambari 26 ambacho kinatowa nafasi kwa tume ya Umoja wa Ulaya kupendekeza uwepo wa ulinzi katika nchi moja mwanachama kwa kipindi cha miezi sita ambazo zinaweza kuongezwa na kwa kipindi cha miaka miwili.

Upande wake Ugiriki katika taarifa yake imetupilia mbali tuhuma kwamba haishughulikii majukumu yake kuhusu swala hili, huku ikiweka bayana gharama ambazo tayari zimetumiwa katika kutekeleza jukumu hili.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.