Pata taarifa kuu
UHISPANIA-SERIKALI-SIASA

Uhispania: Podemos kuungana na vyama vya Kisoshalisti

Kiongozi wa chama cha mrengo wa kulia chenye msimamo mkali cha PODEMOS, Pablo Iglesias, Jumapili hii ameungana na muungano wa vyama vya Kisoshalisti wa PSOE ili kuzuia uteuzi wa serikali ya Uhispania inayoundwa na Mariano Rajoy kutoka chama cha Conservative.

Pablo Iglesias kiongozi wa chama cha PODEMOS jijini Madrid, Desemba 21, 2015.
Pablo Iglesias kiongozi wa chama cha PODEMOS jijini Madrid, Desemba 21, 2015. AFP/AFP/
Matangazo ya kibiashara

Mariano Rajoy alishinda uchaguzi wa wabunge mwezi Desemba mwaka jana.

"Hatutoachia uongozi wa Uhispania kwa Mariano Rajoy", Pablo Iglesias, amesema mbele ya Baraza la kiraia, ambalo ni bodi ya uongozi wa chama chake cha PODEMOS.

"Tunapaswa kuendelea kushikamana na" wabunge wa PSOE " wenye busara zaidi" ili kujua "upande waliopo", ameendelea.

Kiongozi wa chama cha PODEMOS amerejelea hata hivyo nia yake ya kuandaa kura ya maoni juu ya uhuru wa Catalonia, kura ambayo vyama vya Kisoshalisti havitaki.

Hata kama PODEMOS, chama cha kisiasa cha tatu chenye watu wengi nchini Uhispania ambacho kilipata viti 69 katika Baraza la Wawakilishi, na muungano wa vyama vya Kisochalisti PSOE (viti 90) vilitangaza kwamba vitapiga kura dhidi ya uteuzi wa Bw Rajoy, pande hizo mbili hazikubaliani juu ya suala la kura la uhuru wa Cataloni, na hivyo kuzuia muungano wowote baina ya pande hizo mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.