Pata taarifa kuu
ULAYA-MWAKA 2015

Mwaka Mpya: maadhimisho chini ya ulinzi mkali

Katika masaa machache yajayo, mwaka 2015 utakua umeondoka na kuingia mwaka mpya wa 2016 . Katika mji wa Paris, maelfu ya watu watasherehekea Mwaka Mpya katika eneo la Champs Elysées.

Kanisa kuu la Notre-Dame jijini Paris chini ya ulinzi wa jeshi, 24 Aprili 2015.
Kanisa kuu la Notre-Dame jijini Paris chini ya ulinzi wa jeshi, 24 Aprili 2015. REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

Mwaka 2015 kulishuhudiwa mashambulizi ya kigaidi katika maeneo mbalimbali nchi Ufaransa. Sherehe za leo zitafanyika chini ya ulinzi mkali. Usalama pia umeimarishwa katika nchi nyingi duniani.

• Nchini Ufaransa, vikosi vya usalama viko imara

"Zaidi ya askari polisi na maafisa wa usalama 100,000" wamewekwa katika maeneo mbalimbali nchini kote Ufaransa katika usiku wa kuuaga mwaka 2015 na kuupokea mwaka 2016, mwaka mmoja na nusu baada ya mashambulizi ya mjini Paris na Saint-Denis, Waziri wa mambo ya ndani Bernard Cazeneuve amesema Alhamisi hii. "Hakuna tishio sahihi" la mashambulizi, lakini "tishio kwa ujumla kwa miji mikuu yote ya Ulaya kufuatia ujumbe wa kundi la Islamic State", Bernard Cazeneuve ameongeza.

• Nchini Ubelgiji, Waziri Mkuu amepiga marufuku maadhimisho ya Mwaka Mpya

Hakuna sherehe za sikukuu ya Mwaka Mpya mjini Brussels. Uamuzi huo umechukuliwa na Meya wa mji mkuu wa Ubelgiji uliotolewa Jumatano Desemba 30, baada ya mkutano na mkuu wa polisi. Uamzi huo umechukuliwa kutokana na hatari ya kutokea kwa mashambuliz.

• Nchini Marekani, bado kuna mashaka licha ya utulivu

Katika mji wa New York, sherehe zimeanza kupiga hodi masaa machahe kabla ya kuuaga mwaka 2015.Huku na kule kunashuhudiwa maandalizi mbalimbali, hasa katika eneo la Time Square. Hata hivyo askari polisi wamewekwa katika maeneo mbalimbali kwa kukabiliana na magaidi.

• Nchini Indonesia, tishio haliwahusu tu wageni

Mamilioni ya watu wako mitaa Alhamisi hii jioni kusherehekea Mwaka Mpya nchini Indonesia, nchi yenye Waislamu wengi duniani ambapo polisi pia wamewekwa katika hali tahadhari, hasa katika mji wa Jakarta, ambapo mashambulizi kadhaa yalitibuliwa wiki hii. Askari polisi na wanajeshi 150,000 wamepelekwa katika maeneo mbalimbali nchini humo, ambapo operesheni kubwa za kupambana na ugaidi bado zinaendelea, amearifu mwandishi wetu Jeanne Lefevre.

• Nchini Urusi, wana hofu ya kulengwa tena kwa mashambulizi ya kigaidi

Urusi, pia, imeimarisha ulinzi, hasa katika mji wa Moscow, amearifu mwandishi wetu, Etienne Bouche. Mwaka huu, eneo la Red Square limepigwa marufuku kwa mtu yeyote kufika sehemu hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.