Slovenia yatoa idadi ya wahamiaji 2,500 kuingia kwa siku
Nchi ya Slovenia inasema itaruhusu wahamiaji 2,500 kuvuka mpaka wake kila siku kuelekea katika mataifa mengine ya Ulaya.
Imechapishwa:
Wizara ya Mambo ya ndani imekataa ombi la Croatia kuruhusu wahamiaji zaidi ya elfu tano kuruhusiwa kuingia nchini Slovenia kila siku, kwa sababu nchi ya Austria inayowakaribisha wahamiaji hao inawakubali tu watu 1500 kwa siku.
Imebainika kuwa idaidi kubwa ya wahamiaji hao ni raia wa Afganistan, Syria na Iraa na wanapitia nchi ya Croatia na Slovenia kwenda katika matfa ya Austria na Ujerumani ambayo yanawakubali.
Viongozi wa Umoja wa Ulaya wameshidnwa kufikia mwafaka wa namna ya kukabiliana na wimbi la wahamiaji wanaoingia katika barani hilo.