Pata taarifa kuu
UTURUKI-IS-PKK-USALAMA

Uturuki: vikwazo vya kwanza vyachukuliwa baada ya mashambulizi Ankara

Viongozi wa Uturuki wamewafuta kazi Jumatano wiki hii wakuu wa polisi mjini Ankara, siku nne baada ya mashambulizi ya kujitoa mhanga yaliyo gharimu maisha ya watu wengi katika historia ya nchi hiyo na kusababisha Rais Recep Tayyip Erdogan kukosolewa vikali na wapinzani wake siku moja kabla ya uchaguzi wa wabunge.

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan akiwasili kwenye eneo la mashambulizi, ambapo ameweka shada la maua.
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan akiwasili kwenye eneo la mashambulizi, ambapo ameweka shada la maua. YASIN AKGUL/Cihan/AFP
Matangazo ya kibiashara

Erdogan alikubali Jumanne uwezekano wa " utovu wa nidhamu " wa Idara zake kabla ya shambulio hilo. Masaa kadhaa baadaye, Wizara ya Mambo ya Ndani ilitangaza kufuta kazi kwa mkuu wa polisi katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kadri Kartal na manaibu wake wawili wanaohusika na Ujasusi na Usalam wa raia.

Uamuzi huu umechukuliwa ili " kuwezesha uchunguzi " imeeleza wizara ya Mambo ya Ndani katika taarifa yake.

Kwa mara ya kwanza akionekana hadharani tangu kutokea kwa mashambulizi hayo, Rais Erdogan ametangaza ufunguzi wa uchunguzi na Bodi ya Wakaguzi wa Nchi (DDK) ili kutambua uwezekano wa kutowajibika kwa Usalama kabla ya mashambulizi, ambayo yaligharimu maisha ya watu 97 na zaidi ya 500 kujeruhiwa Jumamosi wiki iliyopita.

Kwa siku tatu, Rais Erdogan ameendelea kukosolewa na wapinzani wake, ikiwa ni pamoja na upinzani unaounga mkono Wakurdi ambao wanamnyooshea kidole kuhusika katika mashambulizi hayo.

Watuhumiwa watambuliwa

Tangu Jumamosi wiki iliyopita, maelfu ya watu waliandamana nchini Uturuki, na kupiga kelele " Tayyip muuaji " ili kukemea mkakati wa mvutano uliotekelezwa na rais huyo, kwa mujibu wa waandamanaji.

Rais Erdogan amewasili Jumatano asubuhi wiki hii eneo la tukio, ambapo aliweka shada la maua katika eneo la kumbukumbu la waathirika.

Viongozi wa Uturuki wamelinyooshea kidolea kundi la Islamic State (IS) kwamba ni "mtuhumiwa namba moja" wa mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga yaliyotokea Jumamosi wiki iliyopita katika kituo kikuu cha magari mjini Ankara. Bila kwenda mbali, Rais Erdogan alisema Jumanne usiku kwamba " mashambulizi ya kigaidi asili yake ni Syria."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.