Pata taarifa kuu
UFARANSA, UJERUMANI-UHISPANI-AJALI-USALAMA WA ANGA

Airbus A-320: zoezi la kutafuta miili lasitishwa usiku

Zoezi la kutafuta miili ya abiria waliouawa katika ajali ya ndege chapa Airbus A- 320 ya shirika la ndege la Ujerumani la Germanwings limeendelea kutatizwa na hali mbaya ya hewa.

Helikopta ya polisi karibu na eneo la tukio, Machi 24 mwaka 2015.
Helikopta ya polisi karibu na eneo la tukio, Machi 24 mwaka 2015. REUTERS/Robert Pratta
Matangazo ya kibiashara

Ndege hiyo ilianguka Jumanne wiki hii katika milima ya Alpes kusini mwa Ufaransa ikiwa na abiria 150 wakiwemo marubani wawili na wahudumu wanne.

Vifaa “ maalumu vya uchunguzi na uokozi” vimetumwa katika eneo la tukio baada ya ajali ya ndege hiyo. Maafisa mia tatu wa Idara ya huduma za dharura na askari polisi mia tatu wametumwa katika eneo la tukio. Helikopta kumi pamoja na ndege ya kijeshi vimetumwa pia katika eneo la tukio.

Hata hivyo zoezi la kutafuta miili ya abiria waliofariki katika ajali hiyo limesitishwa usiku wa kuamkia Jumatano wiki hii. Lakini polisi imebaki katika wigo wa eneo la tukio ikiwa na matumaini ya kusikia kelele yoyote na kuhifadhi mazingira.

Airbus A-320 imekua ikifanya safari kati ya Barcelona na Düsseldorf. Rais wa Ufaransa François Hollande ameeleza kuwa tukio hilo limetokea katika eneo ambalo ni vigumu kuingia, lenye theluji na milima.

Wakati huohuo kisanduku cheusi kinachorekodi mawasiliano katika ndege kimepatikana. Wachunguzi wanaamini kwamba huenda hali mbaya ya hewa au kugongana na ndege nyingine ndio imesababisha ajali hiyo.

Abiria 146 pamoja na marubani wawili na wahudumu wanne waliokua katika ndege hiyo, wote wamefariki. Abiria hao ni kutoka Uhispania, Ujerumani, Ufaransa na Uturuki. Theluthi moja ya abiria hao ni kutoka Uhispania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.