Pata taarifa kuu
UGIRIKI-UCHUMI

Ugiriki yajiondoa kwenye mazungumzo

Mkutano wa mawaziri wa fedha kutoka nchi zinazotumia sarafu ya Yuro, ambao ukikua ukijadili hali ya kiuchumi inayojiri nchini Ugiriki ulidumu kwa masaa machache tu Jumatatu Februari 16 na kumalizika bila hata hivyo kufikia maelewano.

Waziri wa Fedha wa Ugiriki, Yanis Varoufakis,  alionya kuwa Ugiriki iko katika hali ya hatari kiuchumi.
Waziri wa Fedha wa Ugiriki, Yanis Varoufakis, alionya kuwa Ugiriki iko katika hali ya hatari kiuchumi. REUTERS/Alkis Konstantinidis
Matangazo ya kibiashara

Lakini jinsi hali inavyokwenda ndivyo muda uliyotolewa kwa kuikoa Ugiriki unavyofikia kikomo.

Mradi uliyotolewa na nchi zinazotumia sarafu ya Yuro ulionekana na Ugiriki kuwa "haufai" na " haukubaliki", kwani ilikua suala la kuendelea na mpango wa misaada kwa sasa. " Katika mazingira haya, makubaliano yoyote hayawezi kufikiwa kwa leo", Ugiriki imeongeza kusema.

Serikali ya Ugiriki imeleezea imani yake kwamba mkataba kuhusu madeni yake, utafikiwa ndani ya saa arobaini na nane, licha ya kupinga muda wa mwisho uliowekwa na nchi za Ulaya zinazotumia sarafu ya Yuro.

Mkutano huo uligubikwa na hali ya sintofahamu kabla ya kuanza, kwani kila mmoja amekua anapania kushikilia msimamo wake. Waziri wa fedha wa Ugiriki, Yanis Varoufakis, alikua amethibitisha katika jarida la New York Times, kwamba ugiriki imefikia hatua ambayo haiwezi kujikwamua kiuchumi.

Serikali ya Ugiriki inataka kumaliza masharti iliyowekewa katika deni lake la Yuro bilioni mia mbili na arobaini. Lakini bila ya fedha za nyongeza kufikia mwishoni mwa mwezi, inaweza kukosa fedha.

Waziri wa fedha wa Ugiriki, Yanis Varoufakis, amesema Ulaya itafanya "ulaghai uliozoeleka" kwa kutumia mkataba usio na ufumbuzi wa hali iliyopo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.