Pata taarifa kuu
UKRAINE-UFARANSA-UJERUMANi-URUSI-MAPIGANO-USALAMA

Mapigano yarindima Debaltseve

Rais wa Ufaransa, kansela wa Ujerumani na rais wa Ukraine wanatiwa wasiwasi na mapigano yanayoendelea mashariki mwa Ukraine hususan pembezoni mwa mji wa Debaltseve.

Mapigano ynaendelea pembezoni mwa mji wa Debaltseve licha ya makubaliaono ya kusitisha mapigano yaliyoafikiwa. Maelfu wa wanajeshi wa Ukraine wamezingirwa katika mji huo wa mashariki mwa Ukraine.
Mapigano ynaendelea pembezoni mwa mji wa Debaltseve licha ya makubaliaono ya kusitisha mapigano yaliyoafikiwa. Maelfu wa wanajeshi wa Ukraine wamezingirwa katika mji huo wa mashariki mwa Ukraine. REUTERS/Gleb Garanich
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wameyasema hayo baada ya mazungumzo yao kwa simu Jumatatu mchana, kwa mujibu wa Ikulu ya Ufaransa

Jeshi la Ukraine na waasi wanaotaka kujitenga kwa eneo la mashariki wamekua wakituhumiana kila upande kukiuka makataa ya kusitisha mapiano ambayo yalianza kutekelezwa Jumapili Februari 15 usiku. Hali hii imezuia zoezi la kuondoa silaha za kivita katika uwanja wa mapigano kama walivyoafikiana kwenye makubaliano yaliyofikiwa katika mji wa Minsk juma lililopita.

Debaltseve imekua ni mji muhimu mashariki mwa Ukraine. Maelfu ya wanajeshi wa Ukraine wamepiga kambi katika mji huo, na inasadikiwa kuwa wamezingirwa na kambi ya upinzani. Kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa, mapigano yamekua yakiendelea Jumatatu wiki hii pembezoni mwa mji huo.

Rais wa Ufaransa, François Hollande, kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa Ukraine Petro Porochenko wameelezea wasiwasi wao juu ya mapigano hayo. Katika mazungumzo yao kwa simu, viongozi hao wameelezea pendekezo lao la “ kutaka waangalizi wa jumuiya ya usalama na maendeleo barani Ulaya kuwa uhuru kwa kuendelea na kazi yao ipasavyo katika eneo hilo la mashariki mwa Ukraine na kutaka pande husika katika vita vinavyoendelea kuweka chini silaha", kulingana na taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Ufaransa. Viongozi hao watatu wanaomba pia waangalizi wa Jumuiya hiyo " kuwa na vifaa vinavyohitajika kwa kutekeleza wajibu wao".

Umoja wa Ulaya kwa upande wake, umetoa wito kwa pande zote husika kusitisha mapigano mara moja. Sharti kwa ajili ya kudumisha amani ambayo inaonekana ni suala tete kwa sasa.

Hata hivyo Urusi imeendelea kuzituhumu nchi za magharibi kuzuia mchakato wa amani nchini Ukraine. Mshauri wa masuala ya kidiplomasia nchini Urusi, Iouri Ouchakov amesema moja ya tishio kwa azimio la mgogoro ni vikwazo vya nchi za magharibi ziliyoiwekea Urusi, ambapo vikwazo vya mwisho vilianza kutekeleza tarehe 16 Februari. Kwa mujibu wa Ushakov, vikwazo hivi ni kinyume na sheria na vinarudisha nyuma maendeleo ya uhusiano kati ya Urusi na Umoja wa Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.