Pata taarifa kuu
UKRAINE-URUSI-UFARANSA-UJERUMANI

Poroshenko aonyesha paspoti za wanajeshi wa Urusi

Jumamosi wiki hii, rais wa Ukraine, Petro Poroshenko, katika mkutano wa kimataifa kuhusu usalama, mjini Minich, ameonyesha paspoti na vitambulisho vya uraia vya wanajeshi wa Urusi walioingia nchini Ukraine.

Rais Ukraine Poroshenko aonyesha paspoti na vitambulisho vya uraia ili kuthibitisha uwepo wa majeshi ya Urusi nchini Ukraine, katika mkutano wa kimataifa kuhusu usalama, Munich tarehe 7 Februari mwaka 2015.
Rais Ukraine Poroshenko aonyesha paspoti na vitambulisho vya uraia ili kuthibitisha uwepo wa majeshi ya Urusi nchini Ukraine, katika mkutano wa kimataifa kuhusu usalama, Munich tarehe 7 Februari mwaka 2015. REUTERS/Michael Dalder
Matangazo ya kibiashara

Rais Poroshenko, amebaini kwamba hali hiyo inaonyesha jinsi gani Urusi imeendelea na uchokozi na kuendeleza machafuko kwa kuingiza wanajeshi wake nchini Ukraine kwa kuwasaidia waasi wanaotaka kujitenga kwa eneo la mashariki la nchi hiyo.

Rais wa Ukraine amesema ameamua kuleta paspoti na vitambulisho hivyo vya uraia ili kuonesha vithibitisho tosha kuwa Urusi ina mkono katika vita vinavyoendelea mashariki mwa Ukriane.

“ Nimeleta paspoti na vitambulisho vya uraia vya wanajeshi wa Urusi, husuan, maafisa wa Urusi, ambao waliingia nchini Ukraine (...). Huu ni ushahidi tosha unaothibitisha uchokozi wa Urusi na kuwepo kwa wanajeshi wake katika ardhi ya Ukraine," rais Petro Poroshenko amethibitishia viongozi wanaoshiriki katika mkutano kuhusu usalama unaofanyika Munich.

Rais wa Ukraine, Petro Poroshenko, amebaini kwamba, Urusi imekua ikiingiza silaha mbalimbali, makombora, vifaa mbalimbali vya kijeshi pamoja na magari yake ya kijeshi katika ardhi ya Ukraine.

Poroshenko amelani kitendo cha Urusi cha kuingiza vifaa hivyo vya kijeshi ambavyo vimekua vikiwaua wanajeshi na raia wa kawaida wa Ukraine.

Akizungumzia kuhusu mazungumzo ambayo yameanzishwa kati ya Angela Merkel, François Hollande na Vladimir Putin, Poroshenko amesema : “ Tunahitaji kitu rahisi tu, mapigano yakomeshwe”.

“ Unaweza ukafikiria nani katika karne hii ya 21, mtu ambaye anaweza kukinzana na uamzi huu?”, Poroshenko ameuliza.

“ Hatuhitaji operesheni ya kusimamia amani, lakini tunahitaji mapigano yasitishwe, wanajeshi wa kigeni wa Urusi waondolewe katika ardhi ya Ukraine”, ameongeza rais Poroshenko, huku akibaini kwamba iwapo Urusi itawaondoa wanajeshi wake kwenye mpaka na eneo linalodhibitiwa na waasi wanaotaka kujitenga na Kiev, hali ya utulivu na amani itarejea ndani ya majuma kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.