Pata taarifa kuu
UFARANSA-UJERUMANI-UKRIANE-URUSI-DIPLOMASIA

Ukraine: ziara ya Hollande na Merkel Kiev

François Hollande ameifanya ziara ya ghafla mjini Kiev Alhamisi Februari 5 katika jaribio la kupata ufumbuzi, kupitia mazungumzo, wa vita vinavyoendelea kushuhudiwa mashariki mwa Ukraine.

Rais wa Ukraine, Petro Porochenko (katikati), rais wa Ufaransa, François Hollande (kulia) na kansela wa ujerumani Angela Merkel (kushoto) wakiwa mjini Kiev, Ukraine.
Rais wa Ukraine, Petro Porochenko (katikati), rais wa Ufaransa, François Hollande (kulia) na kansela wa ujerumani Angela Merkel (kushoto) wakiwa mjini Kiev, Ukraine. REUTERS/Valentyn Ogirenko
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa ameambatana katika ziara hiyo na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel. Ikiwa ni jaribio la mwisho kwa kuepuka ongezeko la machafuko kati ya Kiev na Moscow.

Hii ni jitihada muhimu ya kidiplomasia tangu kuanza kwa vita mashariki mwa Ukraine. Angela Merkel na François Hollande wanakutana mjini Kiev na rais wa Ukraine, Petro Poroshenko.

Viongozi hao wawili wanatazamiwa kujielekeza Urusi Ijumaa wiki hii kwa mazungumzo na rais wa Urusi, Vladimir Putin. Hatua hiyo inakuja katika mazingira ya kunyoosheana kidole kati ya Urusi na Ukraine wakati ambapo mataifa ya magharibi, ambayo ni washirika wa Ukraine wakihoji kuhusu kiwango chao cha kuhusika katika migogoro hiyo.

Marekani imepania kutoa silaha kwa jeshi la Ukraine. Hii ni moja ya sababu za ziara ya Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, anayoifanya tangu mapema Alhamisi asubuhi wiki hii.

Kwa upande wake, Hollande ameelezea katika mkutano na waandishi wa habari Alhamisi mchana wiki hii, msimamo wa Ufaransa kuipa silaha Ukraine: " Ufaransa haina nia ya kushiriki katika njia hii, angalau kwa sasa", amesema rais Hollande.

“ Njia pekee ya kidiplomasia ndio bado inapewa kipaumbele, na kwa hio Paris na Berlin wamejitenga na msimamo huo wa Washington kwa sababu Marekani inafikiriwa kutoa vifaa vya kijeshi kwa kupambana na waasi wanaotaka kujitenga katika maeneo ya mashariki:, ameongeza Hollande.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.