Pata taarifa kuu
UFARANSA-UJERUMANI-UKRIANE-URUSI-DIPLOMASIA

Ukraine: Hollande na Merkel ziarani Moscow

Rais wa Ufaransa, François Hollande na kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, wanatazamiwa kujielekeza Moscow, nchini Urusi kukutana kwa mazungumzo na rais wa Urusi Vladimir Putin.

Hollande na Kansela wa ujeruman, Angela Merkel wakijiandaa kujielekeza Moscow, nchini Urusi.
Hollande na Kansela wa ujeruman, Angela Merkel wakijiandaa kujielekeza Moscow, nchini Urusi. REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Wawili hao wameanza ziara yao hii tangu Alhamisi wiki hii, ambapo jana jioni waliwasili katika mji mkuu wa Ukraine, Kiev, ikiwa ni hatua ya kwanza ya ziara yao.
Viongozi hao wawili wanajaribu kutafutia ufumbuzi kupitia mazungumzo suala la machafuko yanayoendelea kushuhudiwa mashariki mwa Ukraine.

Hii ni jitihada muhimu ya kidiplomasia tangu kuanza kwa vita mashariki mwa Ukraine. Angela Merkel na François Hollande, baada ya kukutana kukutana kwa mazungumzo na rais Petro Poroshenko mjini Kiev, wanatazamiwa kuendelea na ziara yao hadi Moscow, ambapo itakua hatua ya mwisho ya ziara yao.

Hatua hii inakuja katika mazingira ya kunyoosheana kidole kati ya Urusi na Ukraine wakati ambapo mataifa ya magharibi, ambayo ni washirika wa Ukraine wakihoji kuhusu kiwango chao cha kuhusika katika migogoro hiyo.

Marekani imepania kutoa silaha kwa jeshi la Ukraine. Hii ni moja ya sababu za ziara ya Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, anayoifanya tangu mapema Alhamisi asubuhi wiki hii, licha ya kuwa amebaini kwamba suala la kidiplomasia linapewa kipaumbele kwa kukomesha machafuko hayo.

Alhamisi wiki hii katika mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya Elysée, mjini Paris, Hollande ameelezea msimamo wa Ufaransa kuhusu kuipa silaha Ukraine: " Ufaransa haina nia ya kushiriki katika njia hii, angalau kwa sasa", amesema rais Hollande.

“ Njia pekee ya kidiplomasia ndio bado inapewa kipaumbele, na kwa hio Paris na Berlin wamejitenga na msimamo huo wa Washington kwa sababu Marekani inafikiriwa kutoa vifaa vya kijeshi kwa kupambana na waasi wanaotaka kujitenga katika maeneo ya mashariki”, ameongeza Hollande.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.