Pata taarifa kuu
CANADA

Polisi nchini Canada wamkamata mtuhumiwa aliyeua askari watatu

Polisi nchini Canada imetangaza kuwa inamshikilia raia mmoja anayetuhumiwa kuhusika na mauaji ya polisi watatu na kujeruhi wengine kadhaa kwenye eneo la Moncton mjini New Brunswick.

Justin Bourque mtuhumiwa aliyekamatwa akihusishwa na yhuma za mauaji ya askari polisi watatu wa Canada
Justin Bourque mtuhumiwa aliyekamatwa akihusishwa na yhuma za mauaji ya askari polisi watatu wa Canada Reuters
Matangazo ya kibiashara

Polisi kwenye mji wa New Brunswick kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter leo asubuhi wameandika kuwa Justin Bourque alikamatwa usiku wa kuamkia leo kwenye eneo la Moncton.

Asakri wa kikosi maalumu (SWAT) wa Canada wakiwa kwenye msako wa mtuhumiwa Justin Bourque hapo jana
Asakri wa kikosi maalumu (SWAT) wa Canada wakiwa kwenye msako wa mtuhumiwa Justin Bourque hapo jana Reuters

Taarifa ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyu imetolewa baada ya kufanyika kwa operesheni kubwa na ya kina na polisi wa Canada kuendesha msako wa kumkamata Bourque.

Shule na ofisi za Serikali zilikuwa zimefungwa kwenye mji huo na wananchi walitakiwa kutotembea hovyo usiku na kujifungia majumbani mwao kwakuwa mtuhumiwa huyu alikuwa amejihami kwa silaha nzito.

Kwenye taarifa yao, Polisi kwenye mji wa Moncton wameataka wananchi hivi sasa kutoka kwenye nyumba zao kwakuwa tishio la usalama limemalizwa.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hili wamesema kuwa walishuhudia Polisi wakimkamata mtuhumiwa huyu na kumchukua kwa gari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.