Pata taarifa kuu
Romania

Rais wa Romania aponea chupuchupu katika kura ya kutokuwa na imani naye

Rais wa Romania Traian Basescu ameponea chupuchupu baada ya matokeo ya kura ya kutokuwa na imani nae kuonyesha kwamba asilimia 46,13 ndio walioshioriki uchaguzi huo ambapo hadi sasa asilimia 97 ya vituo vya kupigia kura ndivyo ambavyo tayari vimehesabiwa. Sheria za katiba nchini humo zinaarifu kuwa asilimia ya washiriki inatakiwa kuzidi asilimia 50 ili kura ya kutokuwa na imani naye iweze kupitishwa.

Rais wa Romania Trian Basescu
Rais wa Romania Trian Basescu REUTERS/Bogdan Cristel
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na takwimu zilizotolewa, kwa asilimia 78 ya vituo vya kupigia kura, idadi ya walioshiriki kura hiyo ya maoni imefikia 46, idadi ambayo ni ndogo kuruhusu kutekelezwa kwa kura hiyo ya kutokuwa na imani na rais Traian Basescu ambae anarejea tena kuwa rais wa Romania

mahakama ya kikatiba itathibitisha matokeo hayo kabla ya bunge, wakati ambapo baadhi ya wabunge wanataka bunge lisikubali matukio hayo ya kura ya maoni na kuendelea na harakati za kuhakikisha rais huyo anaondoka madarakani, huku wengine wakiona kwamba kutumia mbinu hizo ni hatari sana kwa taifa hilo katika Umoja wa Ulaya

Traian Basescu ameahidi kudumisha mshikamano baina ya wananchi wa Roumania iwapo atapata nafasi ya kuendelea kuwa rais, jambo ambalo watafiti wanaona kuwa litakuwa gumu sana kwake, kwakuwa licha ya kura ya kutokuwa na maoni naye kutopasishwa asilimia 90 ya waliopiga kura wamempinga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.