Pata taarifa kuu
UKRAIN

Nchi ya Ukrain yaahirisha kuandaa mkutano wa 18 wa viongozi wa mataifa ya Umoja wa Ulaya EU

Serikali ya Ukrain imetangaza rasmi kusitisha kufanyika kwa mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa Ulaya uliopangwa kufanyika juma hili nchini humo kufuatia baadhi ya mataifa kutishia kususia mkutano huo.

Waziri mkuu wa zamani wa Ukrain, Yulia Tymoshenko
Waziri mkuu wa zamani wa Ukrain, Yulia Tymoshenko Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hatua ya nchi hiyo kuamua kufuta mkutano huo kufanyika nchini mwake imekuja baada ya baadhi ya mataifa ya Umoja huo kudai kuwa yangesusia mkutano huo yakipinga unyanyasaji ambao anafanyiwa waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Yulia Tymoshenko anayetumikia kifungo gerezani.

Nchi ambazo zilikwisha tangaza wazi kutohudhuria mkutano huo ni pamoja na Ujerumani, Romania, jamhuri ya Cheki na nchi ya Austria ambazo ziliituhumu mamlaka nchini Ukrain kumnyanyasa kiongozi huyo.

Uamuzi wa serikali ya Ukrain umetangazwa na msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje wa nchi hiyo Oleksandr Dykusarov aliyedai nchi hiyo kutokuwa tayari kuandaa mkutano wa 18 wa viongozi wa nchi za Umoja wa ulaya uliopangwa kuanza nchini humo tarehe 11 hadi 12 ya mwezi huu mjini Yalta.

Mataifa mengi ya Ulaya pia yametishia viongozi wake kutohudhuria sherehe za ufunguzi wa michuano ya EURO iliyopangwa kuanza nchini humo mwezi mmoja ujao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.