Pata taarifa kuu
Ufaransa-Uchaguzi

Francois Hollande na Nicolas Sarkozy kupambana kwenye duru ya pili ya uchaguzi

Duru ya kwanza ya uchaguzi nchini Ufaransa imemalizika ambapo mgombea urais kupitia chama cha kisocialist Francois Hollande ameibuka mshindi kwenye awamu hii ya kwanza kwa kujipatia asilimia 28,63% na kumshinda rais wa sasa wa nchi hiyo Nicolas Sarkozy  kwa asilimia 1,55% ambae alipata asilimia  27,08%. 

François Hollande (G) na Nicolas Sarkozy,
François Hollande (G) na Nicolas Sarkozy, Reuters/Montage RFI
Matangazo ya kibiashara

Ni ushindi ambao wachambuzi wa masuala ya siasa wanadai kuwa ulitabiriwa kwa mgombea Francoisi Hollande kuweza kuibuka mshindi kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi huo dhidi ya mgombea toka chama cha mrengo wa kulia rais Nicolas sarkozy.

Matokeo yaliyotangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi nchini humo yameonesha mgombea Francosi Hllande akipata ushindi wa asilimia 28.63 akifuatiwa kwa ukaribu na rais wa sasa Nicolas Sarkozy aliyepata asilimia 27.08, tofauti ya asilimia 1.55 tu ya kura

Matokeo hayo ambayo yameonekana kuwashangaza wengi yameshuhudia mgombea pekee ambaye ni mwanamke kwenye kinyang'anyiro hicho Marine Le Pen akishika nafasi ya tatu kwa kupata asilimia 18 huku mgombea Jean-Luc Melenchon akishika nafasi ya nne.

Matokeo hayo sasa yanawafanya wagombea wawili Francois Hollande na Nicolas Srakozy kuingia kwenye duru ya pili ya uchaguzi huo ambao unatarajiwa kufanyika tarehe 6 ya mwezi wa tano.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi wa duru ya kwanza ya uchaguzi, mgombea Francois Hollande amesita kusema kuwa atapata ushindi kwenye uchaguzi wa awamu ya pili badala yake amesema ushindi unakaribia.

Kwa upande wake rais Nicolas sarkozy amekiri kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni mgumu lakini hajakata tamaa kushindana kwenye duru ya pili na kwamba anamatumaini ya kuibuka mshindi.

Francois Hollande mgombea wa chama cha Socialist amepata uungwaji mkono wa mgombea alishika nafasi ya nne Jean-Luc Mélenchon ambae alipata asilimia 11,13%, na tayari amewatolea wito wafuasi wake kumpigia kura Francois Hollande kwenye duri ya pili ya uchaguzi huo, ili kumuangusha Sarkozy, lakini pia mgombea mwingine Eva Joly ambae alipata asilimia 2,28% ametangaza kumuunga mkono mgombea wa chama cha socialist.

Upande wake Nicolas Sarkozy,anaelekea jijini  Tours jumanne hii, akiwa na kibaruwa kigumu cha kushawishi wafuasi zaidi katika kipindi cha siku kumina tano zijazo. ili aweze kushinda katika duru ya pili anatakiwa kuzoa kura za chama cha National Front cha Marine Le Pen aliepata asilimia 18.01, lakini pia anahitaji kura za mgombea aliechukuwa nafasi ya nne Francois Bayrou aliepata asilimia 9.11

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.