Pata taarifa kuu

Wakili wa mmiliki wa mtandao wa Wikileaks Julian Assange akata rufaa mteja wake kupelekwa Sweden

Wakili anayemtetea mmiliki wa mtandao unaoandika habari za uchunguzi wa Wikileaks Julian Assange, Ben Emmerson muda mfupi uliopita kwa mara nyingine rufaa katika mahakama ya mjini London kupinga mteja wake kupelekwa nchini Sweeden kujibu mashtaka ya ubakaji yanaoymkabili.

Reuters
Matangazo ya kibiashara

Wakili huyo akiwa na mteja wake waliwasili katika mahakama kuu ya mjini London na kuwasilisha rufaa yao wakipinga huku ya awali iliyoruhusu Assange kupelekwa nchini Sweeden kujibu mashtaka yanayomkabili akidai kuwa hukumu hiyo haikuwa ya haki.

Katika utetezi wao, wakili Emmerson amepinga waranti iliyotolewa na umoja wa ulaya ya kukamatwa kwa mteja wae akisema kuwa imeshindwa kuweka wazi na kuelezea kwa kina mashtaka halisi yanayomkabili mteja wake na hivyo kuona kwamba hatotendewa haki endapo kesi yake itasikilizwa nchini Sweeden.

Julian Assange anakabiliwa na mashtaka ya ubakaji dhidi ya wanawake wawili wa sweeden madai yaliyofunguliwa mwaka jana mwezi wa Nane, mashtaka ambayo Assange mwenyewe anakanusha kuhusika nayo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.