Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-SIASA-UCHUMI

Cyril Ramaphosa kukabiliana na rushwa

Rais mteule wa afrika kusini ambaye amemrithi mtangulizi wake Jacob Zuma tangu jana Alhamisi siku moja baada ya Zuma kujiuzulu , amesema rushwa ni changamoto kuu ya kwanza ambayo atakabiliana nayo.

Rais mteule wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, wakati akiapishwa mbele ya Bunge, Cape Town, Februari 15, 2018.
Rais mteule wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, wakati akiapishwa mbele ya Bunge, Cape Town, Februari 15, 2018. REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Bw Ramaphosa amesema katika kipindi chake chote kwenye uongozi wa nchi atahakikisha rushwa imetokomezwa.

"Rushwa inatakiwa kushughulikiwa vya kutosha, kwani imekithiri na imeathiri nchi hii, " amesema Rais Ramaphosa.

Kashfa ya rushwa nchini Afrika Kusini imechafua sifa ya chama cha ANC katika uongozi wa miaka tisa wa Jacob Zuma. Zuma amekua akishinikizwa kujiuzulu kufuatia kashfa za rushwa zinazomkabili.

"Haya ni matatizo ambayo tutashughulikia," aliahidi Cyril Ramaphosa mbele ya Bunge, wakati alipoapishwa, jana Alhamisi, Februari 15.

"Nitafanya kazi kwa bidii ili nisipotezi imani kwa wananchi wa Afrika Kusini, " aliongeza Bw Ramaphosa, huku akibaini kwamba atafafanua baadhi ya mapendekezo yake kwa wabunge kuhusiana na suala la rushwa wakati wa hotuba yake ya kwanza kuhusu taifa hilo leo Ijumaa jioni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.