Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-JACOB ZUMA

Kashfa tano zilizomkabili rais wa zamani Jacob Zuma

Kujiuzulu kwa Rais Jacob Zuma kumegubikwa na kushinikizwa na changamoto nyingi hasa kashfa kubwa tano ambazo zimeendelea kumkabili.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ambaye pia ni kiongozi wa chama cha ANC, 17 Desemba 2017
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ambaye pia ni kiongozi wa chama cha ANC, 17 Desemba 2017 REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Jacob Zuma mwenye umri wa miaka 75 aliyeingia madarakani 2009 amekua akituhumiwa kwa kashifa nyingi za rushwa.

Kabla ya kkuwa rais wa Afrika Kusini Zuma alifikishwa mahakamani mwaka 2006 akikabiliwa na tuhuma za ubakaji baada ya kufanya mapenzi na mwanamke aliyekua na umri wa miaka 31.

Zuma kuhusu kashifa hiyo alikiri kufanya mapenzi yasiyo salama bila kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi yaani ngono zembe lakini, hakupatikana na kosa lolote na Mahakama.

Ukarabati wa Makaazi ya Nkandla -

Mwaka 2014 akiwa madarakani Zuma alikumbwa na kashifa ya kutumia fedha za walipa kodi wa Afrika Kusini dola milioni 24 kukarabati makazi yake binafsi katika kitongoji cha Kandla kwenye jimbo la KwaZulu-Natal. Hata hivyom alidai kuwa alirejesha fedha hizo.

Familia ya Gupta -

Huku mjadala mkali ukiendelea kuhusu matumizi mabaya ya fedha hizo za UMMA Zuma aliingia katika kashifa nzito maarufu kama Guptagate akituhumiwa kujihusisha na familia ya kibepari ya kihindi ya Gupta,  familia ambayo ilikua na ushawishi mkubwa katika serikali ya Rais Zuma na hata kupata zabuni nyingi za Serikali.

Biashara ya silaha-

Mwaka 2017 mahakama ya juu ya rufaa nchini Afrika ilimua kuwa Zuma alikua na kesi za kujibu za makosa takribani 800 ya rushwa akihusishwa na mkataba wa masuala ya silaha wa mwaka 1990 ambao ulikuja kusainiwa 1999 Zuma akiwa tayari makamu wa Rais.

Omar al-Bashir

Kama kwamba hiyo haitoshi,  Mahakama ya juu ya Afrika Kusini kunako mwezi Machi mwaka 2016 ilitoa uamuzi kuwa hatua ya serikali ya rais  Zuma wakati huo, kushindwa kumakamata rais wa Sudan anayesakwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita- ICC Omar Al  Bashir ilikua kinyume cha Sheria za nchi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.